mapendekezo ya muundo wa sera ya elimu … · web viewvitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya...

149
RASIMU JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI SERA YA ELIMU NA MAFUNZO 2010

Upload: others

Post on 06-Mar-2020

4 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

RASIMU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

SERA YA ELIMU NA MAFUNZO 2010

(Toleo Jipya) JANUARI, 2010

Page 2: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

RASIMU

VIFUPISHO

ADEM Agency for Development of Education Management

AZAKI Asasi za Kiraia DED District Executive DirectorDEOEACEFA

District Eduction Officer East African CommunityEducation For All

EMACESDPEWWENMRA

Educational Materials Approval CommitteeEducation Sector Development ProgrammeElimu ya Watu WazimaElimu Nje ya Mfumo Rasmi

HESLBKCMKCK

Higher Education Students’ Loans BoardKisomo Chenye ManufaaKisomo Cha Kujiendeleza

KKK Kusoma, Kuandika na KuhesabuMDGsMEMKWA

Millenium Development GoalsMpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa

MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania

MMEJU Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya JuuMMEM Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya MsingiMMESMMEUMUKEJA

Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya SekondariMpango wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi StadiMpango wa Uwiano Kati ya Elimu ya watu wazima na Jamii

NACTE National Council for Technical Education

i

Page 3: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

NECTANERNEQANEQF

National Examinations Council of TanzaniaNet Enrolment RatioNational Education Qualifications AuthorityNational Education Qualifications Framework

OWM-TAMISEMI Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

RAS Regional Administrative SecretaryREOSADCSDL

Regional Education OfficerSouthern Africa Development CommunitySkills Development Levy

TEATCUTDMS

Tanzania Education Authority Tanzania Commission for UniversitiesTeachers Development and Management Strategy

TEHAMA Teknolojia ya Habari na MawasilianoTEWW Taasisi ya Elimu ya Watu WazimaTIE Tanzania Institute of EducationTLSB Tanzania Library Services BoardTSDTVET

Teachers Service DepartmentTechnical and Vocational Education and Training

UKIMWI Upungufu wa Kinga MwiliniUN United NationsUNDP United Nations Development ProgrammeUNESCO United Nations Educational Scientific and Cultural

OrganisationUPEVET

Universal Primary EducationVocational Education and Training

VETA Vocational Education and Training AuthorityVVU Virusi vya Ukimwi

ii

Page 4: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

iii

Page 5: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

YALIYOMOVIFUPISHO........................................................................iYALIYOMO.......................................................................iiiDIBAJI.............................................................................vi

SURA 1............................................................................11.0 UTANGULIZI.............................................................1

SURA YA 2........................................................................32.0 HALI YA UTEKELEZAJI WA SERA YA ELIMU NA

MAFUNZO................................................................32.1 Utoaji wa Elimu na Mafunzo kabla ya Sera za Elimu

na Mafunzo................................................................32.2 Utoaji wa Elimu na Mafunzo baada ya Sera za Elimu

na Mafunzo................................................................42.3 Mafanikio..................................................................................92.4 Changamoto...........................................................................11

SURA 3...........................................................................133.0 UMUHIMU WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO...........133.1 Usuli.........................................................................133.2 Mabadiliko yaliyojitokeza katika utekelezaji wa Sera

za Elimu na Mafunzo................................................13

SURA 4...........................................................................174.0 FALSAFA, DIRA, DHIMA NA MADHUMUNI YA SERA YA

ELIMU NA MAFUNZO...............................................174.1 Falsafa ya Elimu na Mafunzo....................................174.2 Dira..........................................................................174.3 Dhima......................................................................174.4 Madhumuni ya Jumla ya Sera ya Elimu na Mafunzo.184.5 Madhumuni Mahsusi................................................18

SURA YA 5......................................................................205.0 HOJA ZA SERA NA MATAMKO................................20

iv

Page 6: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.1 Mfumo na Muundo wa Elimu na Mafunzo.................205.2 Mfumo Rasmi wa Elimu na Mafunzo.........................215.3 Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi465.4 Mitaala ya Elimu na Mafunzo...................................495.5 Matumizi ya Lugha katika Elimu na Mafunzo.........................685.6 Upimaji, Tathmini na Utoaji Vyeti.............................735.7 Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu na Mafunzo....................79SURA YA 6......................................................................976.0 ............................................. MASUALA MTAMBUKA

..............................................................................976.1 Utangulizi.................................................................976.2 Jinsia katika Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu na

Mafunzo...................................................................976.3 Elimu ya Mazingira na Afya ya Jamii........................986.4 Elimu ya VVU/UKIMWI na Athari za Matumizi ya Dawa

za Kulevya................................................................996.5 Huduma za Ushauri na Unasihi..............................1006.6 Utawala Bora..........................................................101

SURA YA 7....................................................................1037.0 MUUNDO WA KITAASISI......................................1037.1 Utangulizi...............................................................1037.2 Ngazi ya Taifa........................................................1037.3 Ngazi ya Mkoa........................................................1037.4 Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa..................1047.5 Ngazi ya Kata.........................................................1047.6 Ngazi ya Shule na Vyuo.........................................104

SURA YA 8....................................................................1058.0 MUUNDO WA KISHERIA......................................1058.1 Utangulizi...............................................................1058.2 Vyombo vya Kisheria.............................................1058.3 Baraza la Taifa la Ushauri wa Elimu na Mafunzo....1058.4 Chombo cha Kudhibiti Ubora wa Ualimu................1058.5 Mamlaka ya Taifa ya Sifa Linganifu (National

Education Qualifications Authority - NEQA)...........106

v

Page 7: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

8.6 Bodi ya Huduma za Maktaba (Tanzania Library Services Board - TLSB)...........................................106

8.7 Baraza la Chuo Kikuu.............................................1068.8 Seneti.....................................................................1068.9 Bodi za Vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo vya Elimu ya

Ufundi na Mafunzo.................................................1078.10 Bodi ya Rufaa ya Mkoa...........................................1078.11 Bodi ya Rufaa ya Halmashauri...............................1078.12 Bodi ya Shule na Chuo cha Ualimu........................1078.13 Kamati ya Shule.....................................................107SURA YA 9....................................................................1089.0 MWISHO..............................................................108

vi

Page 8: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

DIBAJI

Elimu na mafunzo bora ni mkakati wa kipaumbele kufikia malengo ya mipango ya maendeleo yaliyowekwa. Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi (MKUKUTA) pamoja na malengo ya Millenia vinaweka wazi umuhimu wa elimu na mafunzo katika kufikia malengo ya mipango hiyo.

Utoaji wa elimu na mafunzo bora unategemea sana sera zilizopo na utekelezaji wake. Sera ambazo zimekuwa zikitumika katika utoaji wa elimu na mafunzo ni Sera ya Elimu na Mafunzo 1995 Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu 1999, Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo 1996. Pamoja na mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa sera hizo, tathmini iliyofanyika mwaka 2008 ilionyesha kuwa kuna maeneo mengi ya sera hizo ambayo hayakutekelezwa ipasavyo kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo ukosefu wa fedha za kutosha na kutokuwa na muundo sahihi wa utekelezaji. Aidha, tathmini hiyo iliibua mahitaji mapya katika elimu na mafunzo yakiwemo uboreshaji wa mitaala, wajibu wa sekta isiyo rasmi katika elimu na mafunzo na umuhimu wa elimu ya ufundi na stadi za ujasiriamali.

Katika juhudi za kuinua ubora wa elimu na mafunzo hapa nchini, Serikali ililazimika kupitia upya Sera za Elimu na Mafunzo ili kukidhi mahitaji ya elimu na mafunzo hapa nchini.

Malengo ya Sera hii ni: Kuinua ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi zote za elimu na

mafunzo; Kuongeza uwezo wa asasi na taasisi za elimu na mafunzo kukidhi

mahitaji yaliyopo;

vii

Page 9: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Kutoa elimu na mafunzo bora katika fani mbalimbali za elimu na mafunzo kukidhi mahitaji ya soko la ajira;

Kuongeza wigo wa kuchangia kikamilifu gharama za elimu na mafunzo. Kutoa elimu kwa usawa kwa maeneo na makundi mbalimbali Kufanya tafiti za kielimu ili maamuzi yazingatie ushahidi wa kisayansi;

na Kufanya ufuatiliaji na tathmini ili kujua mwenendo wa ufanisi na kufanya

maamuzi rekebishi inapobidi. Ili kufikia malengo ya Sera hii kwa ukamilifu inahitaji ushirikiano wa wadau wote wa elimu na mafunzo katika ngazi zote wakiwemo sekta isiyo ya serikali, Asasi za Kiraia (AZAKI) na Washirika katika Maendeleo.

Mwisho, napenda kuwashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika mchakato mzima na kufanikisha kukamilisha Sera hii.

Profesa Jumanne Abdallah Maghembe (Mb)Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

(Inaendelea Kufanyiwa marekebisho)

viii

Page 10: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA 1

1.0 UTANGULIZIElimu ni mjumuisho wa maarifa na ujuzi wa kujitambua na kujiweka sawa katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika mazingira na mabadiliko ya mara kwa mara ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kisayansi na teknolojia. Aidha, elimu ni nyenzo ya kumwezesha mtu kutambua uwezo na wajibu wake kamili katika jamii ambayo hupatikana kwa mchakato wa kufundisha na kujifunza. Mafunzo ni mchakato wa kupata maarifa, kujifunza stadi, za kutenda kazi na mwelekeo.

Utoaji wa elimu na mafunzo unaongozwa na Sera za Elimu na Mafunzo (1995); Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Elimu ya Juu (1999), sera za jumla za kitaifa, makubaliano na itifaki za kikanda na kimataifa. Aidha, utoaji huu wa elimu unazingatia maelekezo ya sera za kisekta, mikakati na programu mbalimbali; pamoja na masuala mtambuka.

Sera za Elimu na Mafunzo zilijikita zaidi katika kuongeza idadi ya wanafunzi shuleni na vyuoni kwa usawa na kukuza ubora wa elimu na mafunzo. Aidha, sera hizi zilisisitiza juu ya ushirikishwaji wa sekta binafsi na washirika wa maendeleo wa ndani na nje; hususan katika uanzishaji na uendeshaji wa shule na vyuo na ugharimiaji wa elimu na mafunzo.

Vilevile, sera hizi zilisisitiza juu ya umuhimu wa kujenga utaifa; misingi ya maadili ya kitaifa; ushirikiano wa kitaifa na kimataifa; utawala wa sheria na kuzingatia Katiba ya nchi na matamko mengine ya msingi ya kimataifa.

Katika kutekeleza sera za elimu na mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu iliandaliwa. Kutokana na programu hiyo, Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM, 2002 - 2006) na Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES, 2004 - 2009) iliandaliwa na

1

Page 11: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

kuanza kutekelezwa. Aidha, Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Juu (MMEJU) na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (MMEU) ipo katika maandalizi. Wakati mipango hii inatekelezwa, maelekezo kadhaa ya Kitaifa yalitolewa ambayo yalisaidia kuongeza kasi ya utekelezaji wa Sera za Elimu na Mafunzo. Hii ni pamoja na Dira ya Maendeleo Tanzania (Vision 2025), Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) na Ilani ya Uchaguzi ya chama tawala CCM ya mwaka 2005.

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa sera za elimu na mafunzo, upungufu ulijitokeza katika maeneo ya mfumo na muundo, uwezo katika uendeshaji, utawala na ugharimiaji. Aidha, kuna masuala ambayo hayakuwamo katika sera, na mengine yameibuka kutokana na mabadiliko mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Ili kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko hayo, sera za elimu na mafunzo zimepitiwa upya na kuhuishwa ili kupata sera ya elimu na mafunzo inayojitosheleza na inayokwenda sambamba na mabadiliko yaliyotokea na yanayoendelea kutokea nchini na ulimwenguni kwa ujumla.

2

Page 12: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA YA 2

2.0 HALI YA UTOAJI WA ELIMU NA MAFUNZO NCHINI

2.1 Utoaji wa Elimu na Mafunzo Kabla ya Sera za Elimu na Mafunzo.Chimbuko la maendeleo ya elimu nchini ni matokeo ya michakato ya falsafa, sera na sheria zilizoanzishwa katika vipindi mbalimbali kabla na baada ya uhuru. Sera za ujumla za kijamii na kiuchumi zimejengeka tangu Uhuru ulipopatikana mwaka 1961. Baada ya uhuru, Serikali ilitunga Sheria ya Elimu Na.83 ya mwaka 1962 iliyofuta Sheria ya Elimu ya mwaka 1927 ambayo iliruhusu utoaji wa elimu na mafunzo kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi, dini na kabila. Katika Sheria na. 83 ya mwaka 1962 Serikali ilielekeza kuwa mitaala, uongozi na ugharimiaji wa elimu na mafunzo ufuate usawa. Aidha, Kiswahili na Kiingereza zilifanywa kuwa lugha za kufundishia shuleni. Sheria na. 50 ya mwaka 1969 iliweka utaratibu wa kuhamishia Serikalini vyuo vya ualimu na shule za mashirika binafsi na ya dini. Mwaka 1972 baadhi ya majukumu ya uendeshaji na usimamizi wa elimu yaliimarishwa chini ya Mpango wa Madaraka Mikoani.

Sheria mbalimbali muhimu zilitungwa ili kuimarisha utoaji wa elimu zikiwemo Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania Na.21 ya mwaka 1973, Sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Na.12 ya mwaka 1975, Sheria ya Taasisi ya Elimu Tanzania Na.13 ya mwaka 1975 na Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978. Tamko la Azimio la Arusha la mwaka 1967 ni chimbuko la falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo ilisababisha yafanyike mabadiliko makubwa katika sera za jumla za kijamii na kiuchumi. Kutokana na Azimio la Arusha, Azimio la Musoma 1974 liliweka mkazo kuhusu Elimu ya Msingi kwa wote (UPE), uchangiaji wa elimu ya juu, kufanyakazi kabla ya kujiunga na chuo kikuu isipokuwa wasichana waliruhusiwa kujiunga moja kwa moja. Falsafa ya Elimu ya Kujitegemea ilianzishwa ili kutekeleza sehemu ya sera za

3

Page 13: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

jumla, ikisisitiza mambo makuu yafuatayo: Kuondoa matabaka katika utoaji elimu na kuwezesha wanafunzi

kuthamini kazi za mikono na kuoanisha waliyojifunza darasani na shughuli za jamii.

Kuondoa utengano (alienation) kati ya shule na jamii na kusaidia kuondoa kasumba ya wasomi ya kujibagua na kutumia elimu waliyoipata kwa maendeleo ya jamii.

Kuunganisha nadharia na vitendo, kwa dhana kuwa elimu isipatikane vitabuni tu bali ijumuishe na ile ipatikanayo kutokana na uzoefu wa kutenda au kufanya kazi za kuongeza tija.

Shule na vyuo kuwa vituo vya kuzalisha ili kuchangia gharama za uendeshaji kwa asilimia ishirini na tano.

Elimu inayotolewa katika kila ngazi iwe na maarifa na stadi za kumwezesha mhitimu kuishi na kufanya kazi yenye manufaa katika jamii

Pamoja na umuhimu wa falsafa ya Elimu ya Kujitegemea, mwelekeo wa utoaji wa elimu na mafunzo uliopo unaegemea zaidi taaluma inayolenga utoaji wa maarifa na stadi kwa nadharia bila kuzingatia vitendo.

2.2 Utoaji wa Elimu na Mafunzo Baada ya Sera za Elimu na MafunzoMfumo wa utoaji wa Elimu na Mafunzo nchini unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996 na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu ya mwaka 1999. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ulipata nguvu kutokana na Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 10 ya mwaka 1995. Serikali inaendelea kuhimiza utoaji wa elimu kwa wote na mafunzo bora ambayo ni msingi wa dhana na dhamira ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Pamoja na juhudi za Serikali kutimiza azma hiyo, mfumo wa elimu uliopo haukidhi mahitaji ya jamii.

4

Page 14: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Katika jitihada za kuimarisha elimu nchini, vyombo mbalimbali viliundwa kama; vile Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ambayo sasa imekuwa Taasisi ya Elimu Tanzania (Tanzania Institute of Education – TIE 1975); Baraza la Mitihani Tanzania (National Examinations Council of Tanzania – NECTA 1973); Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (Institute of Adult Education- IAE 1975); Bodi ya Huduma za Maktaba (Tanzania Library Service Board-TLSB 1975); Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Vocational Education and Training Authority – VETA 1994) ambavyo viliundwa kabla ya Sheria Na. 25 ya mwaka 1978 na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996 na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu ya mwaka 1999. Vyombo hivi, kila kimoja husimamiwa na Bodi ambazo zimeundwa kwa mujibu wa Sheria. Hata hivyo, bodi hizo hazina uhusiano wa kisheria katika utendaji wa majukumu yao. Aidha, uratibu miongoni mwa vyombo hivyo, na kati ya vyombo hivyo na Wizara yenye dhamana ya Elimu ni dhaifu. Vyombo vingine kama Chuo cha Uongozi na Usimamizi wa Elimu ambacho sasa kimekuwa Wakala wa Mendeleo ya Uongozi wa Elimu (Agency for Development of Educational Management – ADEM Act 2001), Tume ya Vyuo Vikuu (Tanzania Comission for Universities-TCU, Universities Act 2005); Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority - The Education Fund Act 2001); Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Higher Education Students’ Loans Board – HESLB Act 2004) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education – NACTE Act Na.9 of 1997) vilianzishwa kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa Sera za Elimu na Mafunzo. Vyombo hivi vina uratibu na mawasiliano hafifu ya Kisheria ya kuoanisha shughuli zao.

Sera ya Elimu na Mafunzo na sera nyingine za elimu zimekuwa zikitekelezwa kwa kuzingatia falsafa ya elimu ya kujitegemea na sera za jumla za taifa ambazo ni Dira ya Maendeleo Tanzania 2025 (Tanzania Development Vision

5

Page 15: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

2025) iliyotangazwa mwaka 1999 na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA) uliotangazwa mwaka 2004. Wakati wa kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (Education Sector Development Programme - ESDP) ilianzishwa mwaka 1997 kwa lengo la kujumuisha mipango ya sekta ndogo za elimu kwa mfumo jumuishi badala ya mfumo wa kila sekta ndogo ya elimu kuwa na mpango wake. Kutokana na Programu hii, Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Sekondari (MMES) iliandaliwa na kutekelezwa. Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Juu (MMEJU) na Elimu ya Ufundi (MMEU) ipo katika hatua za maandalizi. Aidha, utekelezaji wa sera za elimu na Mafunzo ulifanyika kwa kushirikiana na wadau wa kitaifa na kimataifa.

Mfumo na Muundo wa Elimu na MafunzoMfumo wa Elimu na Mafunzo wa Tanzania ni utaratibu wa kutoa elimu na mafunzo ambao umejengwa na muundo wenye mpangilio wa ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Mfumo huu una sehemu kuu mbili, mfumo rasmi na usio rasmi.

Mfumo rasmi wa elimu na mafunzo ni wa kitaaluma na kitaalamu ukianzia ngazi ya elimu ya msingi hadi elimu ya juu. Muundo wa elimu na mafunzo wa kitaaluma unaotumika ni 2-7-4-2-3+: ambapo miaka 2 ya Elimu ya Awali, miaka 7 ni ya Elimu ya Msingi; miaka 4 ni ya Elimu ya Sekondari ya ngazi ya Kawaida; miaka 2 ni ya Elimu ya Sekondari ya Ngazi ya Juu; na miaka 3 au zaidi ni ya Elimu ya Juu. Muundo wa elimu na mafunzo wa kitaalamu unaanza baada ya elimu ya sekondari na inakuwa ya mwaka mmoja (1) au zaidi na kuendelea mpaka elimu ya juu.

Elimu na mafunzo nchini Tanzania husimamiwa na wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo. Wizara nyingine, Taasisi na idara za Serikali na zisizo za Serikali ni wadau katika utoaji wa elimu na mafunzo kwa mfumo rasmi na usio rasmi.

a) Elimu ya Awali

6

Page 16: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Serikali inatambua kuwa elimu ya Awali ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto kimwili, kiakili na kimaadili. Tafiti kadhaa zilizofanyika nchini katika miaka ya 1980 zimebaini kuwa watoto waliopitia elimu ya awali huwa na mafanikio makubwa zaidi wanapojiunga darasa la kwanza.

Kutokana na kutambua umuhimu huu Serikali iliamua kuingiza Elimu ya Awali kwa watoto wenye umri wa miaka 5 na 6 kwenye mfumo rasmi wa Elimu. Baadhi ya watoto wadogo wenye umri chini ya miaka 5 wanalelewa na kupewa elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogo. Kila shule ya msingi inapaswa kuwa na madarasa ya Elimu ya Awali.

b) Elimu ya MsingiElimu ya Msingi inatolewa kwa miaka saba (7) na ni ya lazima kwa uandikishaji na mahudhurio kwa mujibu wa sheria. Baada ya Elimu ya Msingi, baadhi ya wahitimu huendelea na Elimu ya Sekondari, Mafunzo ya Ufundi Stadi; na waliokosa fursa hizo huingia kwenye ulimwengu wa kazi. Elimu ya msingi inatekelezwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya msingi kwa awamu.

c) Elimu ya SekondariElimu ya Sekondari inatolewa kwa miaka 6. Elimu hii imegawanyika katika Ngazi ya Kawaida ya miaka minne ya Kidato cha 1 hadi 4; na Ngazi ya Juu ya miaka miwili ya Kidato cha 5 na 6. Wanafunzi wanaohitimu Elimu ya Sekondari Ngazi ya Kawaida huendelea kwenye Elimu ya Sekondari Ngazi ya Juu; mafunzo ya Kitaalamu; na ulimwengu wa ajira. Waliohitimu Elimu ya Sekondari Ngazi ya Juu hujiunga na taasisi na vyuo vya Elimu ya Juu; na soko la ajira. Elimu ya Sekondari inatekelezwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari kwa awamu.

d) Elimu ya UalimuElimu ya Ualimu inatolewa katika Vyuo vya Ualimu na Vyuo Vikuu vya Serikali na visivyo vya Serikali. Vyuo vya Ualimu vinatoa mafunzo ya Cheti Daraja A kwa Walimu wa shule za Msingi na Stashahada kwa Walimu wa shule za Sekondari Ngazi ya Kawaida. Elimu ya Ualimu ngazi ya cheti inatolewa kwa wahitimu wa Elimu ya Sekondari ngazi ya kawaida na ya

7

Page 17: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

stashahada kwa wahitimu wa Elimu ya Sekondari ngazi ya juu. Vyuo Vikuu vinatoa Walimu kwa ajili ya shule za Sekondari Ngazi ya Juu na Wakufunzi kwa ajili ya Vyuo vya Ualimu. Baada ya kuanza kutekelezwa kwa MMEM na MMES, mahitaji ya walimu yameongezeka. Elimu ya Ualimu inatekelezwa kwa Mkakati wa Maendeleo na Menejimenti ya Walimu (Teachers Development and Management Strategy - TDMS)

e) Elimu ya Ufundi na Mafunzo Elimu ya Ufundi na Mafunzo inaambatana na upataji wa ujuzi kwa ajili ya ajira au kujiendeleza zaidi kiufundi na kitaalamu. Elimu hii ina programu za biashara, ufundi na mafunzo ya kazi yanayoendeshwa na Wizara mbalimbali, mashirika yasiyo ya Kiserikali na taasisi binafsi. Elimu ya Ufundi na Mafunzo hutolewa katika ngazi ya ufundi stadi, ya ufundi sanifu na ngazi ya uhandisi/ uteknolojia. Ngazi ya ufundi stadi hutolewa zaidi na vyuo vinavyosimamiwa au kuratibiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Stadi (VETA). Elimu ya Ufundi na mafunzo ngazi ya ufundi sanifu na uhandisi/ uteknolojia hutolewa na vyuo vya Wizara za sekta husika pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali. Elimu na Mafunzo haya ni muhimu kwa kutoa rasilimaliwatu inayotumika viwandani, mashambani na katika sekta nyingine za uzalishaji na huduma. Ngazi ya ufundi stadi inachukua wanafunzi wanaohitimu Elimu ya Msingi na ya Sekondari. Ngazi ya ufundi sanifu inachukua wanafunzi waliohitimu Elimu ya Sekondari na baadhi ya wahitimu wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ngazi ya ufundi stadi. Elimu katika ngazi hii inaratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Ngazi ya uhandisi/ uteknolojia inachukua wahitimu wa Elimu ya Sekondari ngazi ya uhandisi/ uteknolojia na baadhi ya wahitimu wa Elimu ya Ufundi ngazi ya ufundi sanifu.

f) Elimu ya Juu.Elimu ya Juu ni elimu itolewayo baada ya Elimu ya Sekondari na hutolewa katika vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali katika mfumo rasmi na nje ya mfumo rasmi. Taasisi za elimu ya juu hutoa mafunzo ya kitaalamu na hutuza vyeti, stashahada, shahada, stashahada za uzamili, shahada za uzamili na uzamivu. Taasisi hizi zinawajibika kufundisha, kufanya utafiti, kutoa ushauri wa kitaalamu na kuandaa na kutoa kada za wataalamu wa ngazi ya kati na

8

Page 18: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

ngazi ya juu. Katika kuinua ubora na kupanua Elimu ya Juu vyombo mbalimbali vilianzishwa kwa nyakati tofauti ikiwa ni pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania; Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi; Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na Mamlaka ya Elimu Tanzania.

Elimu Nje ya Mfumo Rasmi na Elimu ya Watu WazimaMfumo usio rasmi umejengwa katika mifumo miwili ambayo ni mfumo unaoratibiwa unaojulikana kama Elimu na Mafunzo Nje ya Mfumo Rasmi; na usioratibiwa.

Elimu na Mafunzo nje ya mfumo rasmi hutolewa kwa watu ambao hawakupata fursa ya Elimu na Mafunzo katika mfumo rasmi. Elimu na Mafunzo ya aina hii, hujumuisha Kusoma, Kuandika, Kuhesabu (KKK) na kujiendeleza baada ya kupata stadi za KKK. Elimu na Mafunzo ya aina hii hutolewa kwa njia ya masafa na ana kwa ana. Mpango wa Uwiano Kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA) hutoa elimu na mafunzo kwa watu wazima kwa ajili ya kuwawezesha kufanya kazi zao katika jamii kwa tija na ufanisi. Aidha, Watoto wenye umri wa miaka 11 – 18 waliokosa Elimu ya msingi kupitia mfumo rasmi huipata elimu hiyo kupitia Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA).

Ugharimiaji wa Elimu na Mafunzo

Serikali kuu kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa hugharimia elimu na mafunzo. Aidha, wazazi, jamii na mashirika wadau wa elimu na mafunzo hushiriki katika kugharimia elimu na mafunzo. Katika juhudi za kuongeza tija na ufanisi mifuko mbalimbali ilianzishwa; Mfuko wa Elimu - mwaka 2001, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Higher Education Students’ Loans Board - HESLB, mwaka 2004) na kodi ya maendeleo ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (Vocational Education and Training - VET Levy) mwaka 1994 ambayo imebadilishwa kuwa Kodi ya Maendeleo ya Stadi (Skills Development Levy - SDL) mwaka 2001.

9

Page 19: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

2.3 MafanikioKatika kutekeleza sera za elimu na mafunzo kumekuwepo na mafanikio mbalimbali kama ifuatavyo: Kurasimishwa kwa elimu ya awali kwa watoto wenye umri wa miaka 5

hadi 6; Kufikia mwaka 2009 asilimia 24 ya watoto walioandikishwa darasa la

kwanza walipitia elimu ya awali; Baada ya kuanza kutekelezwa kwa MMEM, uandikishaji wa watoto wote

wa rika lengwa wa umri wa miaka 7-13 (NER), umeongezeka kutoka asilimia 58.1 mwaka 2001 hadi kufikia asilimia 95.9 mwaka 2009 na uwiano wa wasichana kwa wavulana uliimarika kuwa wastani wa 1:1;

Idadi ya shule za msingi zimeongezeka kutoka 11,873 mwaka 2001 hadi 15,727 mwaka 2009;

Uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi uliimarika kutoka 1:57 mwaka 2000 hadi 1:54 mwaka 2009;

Idadi ya wahitimu wa elimu ya msingi wanaojiunga na Elimu ya Sekondari ngazi ya Kawaida wa rika lengwa imeongezeka kutoka 8.4% mwaka 2004 hadi 29.1% mwaka 2009 na uwiano wa wasichana kwa wavulana katika Ngazi ya Sekondari ya kawaida ulikua kwa wastani wa 1:1 mwaka 2009;

Idadi ya shule za sekondari zimeongezeka kutoka 1,291 mwaka 2004 hadi 4,102 mwaka 2009;

Ili kukidhi mahitaji ya walimu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ilipanua utoaji wa mafunzo ya ualimu kwa kuongeza uandikishaji katika vyuo vilivyopo na kuanzisha vyuo vipya vya ualimu;

Vyuo vikuu vishiriki viwili vya elimu vya serikali vilianzishwa kwa lengo la kutoa walimu wa shahada pekee. Aidha, chuo kikuu kimoja (1) kisicho cha Serikali kinatoa walimu wa shahada pekee na baadhi ya vyuo vingine vya Serikali na visivyo vya Serikali vinatoa programu za elimu ya ualimu;

Vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi vimeongezeka kutoka 819 mwaka 2005 hadi 889 mwaka 2008. Aidha, idadi ya wanachuo imeongezeka kutoka 79,031 mwaka 2005 hadi kufikia 114,295 mwaka

10

Page 20: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

2008; Vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo vinavyotoa elimu ngazi ya cheti,

stashahada, shahada na stashahada ya juu vimeongezeka kutoka 172 mwaka 2005 hadi 223 mwaka 2009;

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education – NACTE) lilianzishwa kwa ajili ya kusimamia ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo;

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (Dar es Salaam Institute of Technology - DIT) na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya Institute of Science and Technology – MIST) na zilianzishwa ili kutoa program za mafunzo ya ngazi ya cheti, stashahada na shahada za sayansi na teknolojia;

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Memorial Academy – MNMA) kwa lengo la kutoa mafunzo ngazi ya cheti, stashahada na shahada za sayansi jamii;

Chuo cha Ufundi Arusha kimepewa mamlaka ya kutoa mafunzo ngazi ya cheti, stashahada na shahada za Uhandisi/ Uteknolojia;

Muundo wa Sifa Linganifu za Elimu ya Ufundi na Mafunzo (TVET Qualifications Framework) umeanzishwa kwa nia ya kuunganisha ngazi ya ufundi stadi na ngazi ufundi sanifu na ngazi ya uhandisi/ uteknolojia;

Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (Vocational Education and Training Authority – VETA) ilianzishwa kusimamia ubora wa mafunzo ya ufundi stadi;

Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka 28 mwaka 2005 hadi 31 mwaka 2009;

Udahili katika vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki umeongezeka kutoka 40,993 mwaka 2005/2006 hadi 95,525 mwaka 2008/2009;

Programu mpya za ujasiriamali, sayansi ya mazingira na teknolojia ya habari na mawasiliano zimeanzishwa katika vyuo vikuu mbalimbali;

Tafiti mbalimbali katika maeneo ya maafa, ardhi, makazi, kilimo na magonjwa mbalimbali na uhifadhi wa mazingira; na

11

Page 21: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Mifuko ya kugharamia elimu na mafunzo ya TEA, SDL na Bodi ya Mikopo imeanzishwa ili kutoa ruzuku na mikopo ya kugharamia elimu na mafunzo. Aidha, jamii imehamasishwa kuchangia gharama za elimu na mafunzo kwa njia mbalimbali.

2.4 ChangamotoIngawa Sera za elimu na mafunzo zimejenga mazingira ya utoaji wa elimu na mafunzo wenye mafanikio, umejitokeza upungufu katika mfumo na muundo na utekelezaji katika maeneo ya: uendeshaji; utawala, usimamizi na ugharimiaji; mawasiliano ndani ya Muundo wa Wizara; na mawasiliano ya kitaasisi. Hali kadhalika, upungufu wa rasilimaliwatu, fedha na vifaa na katika sheria umechangia kudhoofisha utekelezaji wa sera za elimu na mafunzo nchini. Baadhi ya changamoto hizo ni kama ifuatavyo:- Idadi kubwa ya watoto wanaandikishwa darasa la kwanza bila kupata

elimu ya awali; Uandikishwaji mdogo wa wanafunzi katika maeneo yenye mazingira

magumu; Uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi katika ngazi ya sekondari

uliongezeka kutoka 1:23 mwaka 2004 hadi kufikia 1:43 mwaka 2009; mawazo mgando katika jamii kuhusu elimu na mafunzo ya watoto wa

kike na wenye ulemavu; mdondoko mkubwa wa wanafunzi na walimu kuondoka katika kazi ya

ualimu; Uhuishaji wa mitaala na programu za elimu na mafunzo ili kukidhi

mahitaji ya washiriki, jamii na soko la ajira; Uwezo mdogo wa baadhi ya watendaji katika mfumo wa usimamizi na

uendeshaji wa elimu na mafunzo; Ukosefu wa uratibu thabiti wa taasisi mbalimbali na wizara zinazotoa na

kuratibu elimu na mafunzo; Tija na ufanisi mdogo katika mfumo wa utekelezaji wa sera za elimu na

mafunzo;

12

Page 22: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Udahili mdogo wa wanafunzi ikilinganishwa na wenye sifa za kujiunga katika vyuo vya elimu ya juu;

Upungufu wa walimu katika maeneo ya sayansi, hisabati, teknolojia na lugha;

Walimu kutopenda kufanya kazi katika maeneo ya pembezoni; Upungufu, uchakavu wa mitambo, mashine na vifaa vilivyopitwa na

wakati; na uchakavu wa miundombinu katika taasisi za elimu na mafunzo;

Mtazamo hasi wa jamii kuhusu elimu ya ufundi na mafunzo; Mtazamo na mawazo mgando ya ujinsi yanayochangia ushiriki mdogo

wa wasichana na wanawake katika kupata elimu ya ufundi na mafunzo; Uhaba wa wakufunzi wa elimu ya ufundi na mafunzo katika vyuo na

taasisi za elimu ya ufundi na mafunzo; na Kutokuwepo kwa mfumo wa sifa linganifu kitaifa (Natinal Qualifications

Framework) wa kuwezesha wahitimu kutoka elimu ya ufundi na mafunzo kujiendeleza kwa ngazi za juu.

13

Page 23: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA 3

3.0 UMUHIMU WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO

3.1 UsuliSera ni matamko yatokanayo na masuala ya msingi yenye dhamira ya kuelekeza namna ya kukabili changamoto kwa ajili ya maendeleo katika jamii. Aidha, inaweka wazi dira, dhima na kuelekeza juu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, idara, taasisi, sekta binafsi na jamii kwa ujumla. Sera inazingatia Dira ya Taifa na mikakati ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa. Wananchi ndiyo chimbuko, walengwa wakuu, wadau na watekelezaji wa sera.

Sera za Elimu na Mafunzo (1995), Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Elimu ya Juu (1999) zimekuwa zikitumika kwa kipindi cha zaidi ya muongo mmoja. Sera hizo zimetafsiriwa katika mikakati mbalimbali ya utekelezaji. Baadhi ya mikakati hiyo ni Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (Education Sector Development Programme - ESDP), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES). Mikakati hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia maelekezo ya sera na mikakati ya jumla ya kitaifa na kimataifa kama Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025, Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA), Elimu kwa Wote (Education for All - EFA) na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals - MDGs).

3.2 Mabadiliko Yaliyojitokeza Katika Utekelezaji wa Sera za Elimu na Mafunzo.Tangu kuanza kutekelezwa kwa Sera za Elimu na Mafunzo, kumekuwa na mabadiliko mbalimbali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia ambayo yanaleta changamoto katika mipango ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo. Aidha, kuna masuala ambayo yameibuka kutokana na

14

Page 24: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

mabadiliko mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kushawishi kupitiwa kwa sera na mikakati mbalimbali ya Elimu na Mafunzo. Masuala hayo ni pamoja na Utandawazi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Elimu ya Jinsia, Utawala Bora, Stadi za Maisha, Ushauri na Unasihi, Huduma na faraja kwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na wenye UKIMWI, Elimu Jumuishi na Elimu ya Mazingira.

Matamko ya kitaifa, kimataifa na kikanda ambayo yamezingatiwa katika uhuishaji wa Sera za Elimu na Mafunzo ni pamoja na: i) Itifaki ya SADC kuhusu elimu na mafunzo (SADC Protocol on Education

and Training - Blantyre 1997): Kuongeza utoaji na upatikanaji wa elimu na mafunzo bora, yenye

manufaa na kwa usawa; Kuwa na uratibu katika utoaji wa rasilimali mbalimbali za elimu na

mafunzo baina ya serikali, wadau na waajiri; Kujenga ubia katika uendelezaji na uzalishaji wa vifaa vya kufundishia na

kujifunzia; Kuwa na ulinganifu wa sifa za kujiunga na vyuo vya elimu na mafunzo

pamoja na utambuzi rasmi wa tuzo; na Kuleta ulinganifu wa mifumo ya elimu na sifa za wahitimu kikanda ili

wahitimu mahiri wawe huru kutumia elimu na ujuzi wao kwa manufaa ya Taifa na Kanda.

Aidha, kuhusu Elimu ya Ufundi na Mafunzo (TVET) inasisitizwa kuwepo kwa mfumo ambao:-

utakuwa na mtaala unaolenga utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo iliyo bora na inayokidhi mahitaji ya soko la ajira;

utakuwa linganifu, shirikishi na wa kukidhi viwango vinavyotakiwa kitaifa, kikanda na kimataifa;

utachangia kubadilishana uzoefu, mawazo na taarifa ambazo zitajenga msingi na maarifa ya elimu ya ufundi na mafunzo kwa wakufunzi;

utakuwa na upimaji na uthibiti wa elimu ya ufundi na mafunzo; na

15

Page 25: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

utaanzisha vituo maalumu vya utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo kwa lengo la kuendeleza na kutoa programu zinazozingatia mahitaji na mipango ya maendeleo ya nchi.

ii) Elimu kwa Wote (Dakar Framework of Action 2000) ambayo inasisitiza haki ya elimu bora kwa watoto wote bila kujali tofauti zao na watoto wenye ulemavu wajumuishwe kwenye madarasa ya kawaida (Elimu Jumuishi).

iii) Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals - MDGs) ambayo pamoja na kusisitiza ulazima wa kuwa na elimu bora ya msingi kwa wote yanaelekeza juu ya upatikanaji wa elimu ya kujikinga na Virusi vya Ukimwi na Elimu ya Mazingira.

iv) UNESCO_PERTH Declaration, 2007 kuhusu elimu ya Sayansi na Teknolojia inayosisitiza kuwa Sayansi na teknolojia:

iendane na mahitaji ya watu binafsi na jamii; itolewe mapema na kwa usawa; irejewe ili kuweza kupima umahiri wa wanafunzi kwa kushirikisha mbinu

za upimaji za ndani na nje ya shule; itolewe na walimu mahiri wa sayansi na teknolojia; na Walimu wa sayansi na teknolojia waendelezwe.v) Makubaliano katika mkutano mkuu wa UNESCO kuhusu elimu ya ufundi

na mafunzo katika karne ya 21 (Paris 2002):- Elimu ya ufundi na mafunzo ipewe nafasi katika elimu ya jumla (general

education) na ijumuishwe katika mabadiliko (Reforms) ya elimu na mafunzo;

Kuwepo na Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambayo itakidhi matakwa ya mfumo wa sera za jumla (macro policies);

Elimu ya Ufundi na Mafunzo itoe nafasi ya kuwezesha jamii kushiriki mafunzo hayo katika mfumo rasmi na usiorasmi katika maisha yao yote (life-long learning).

vi) Makubaliano ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Elimu na

16

Page 26: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Mafunzo (EAC Treaty on Education and Training). Makubaliano haya yanatamka kwamba kila nchi mwanachama itachukua hatua madhubuti za kuimarisha ushirikiano katika elimu na mafunzo katika maeneo yafuatayo:

Uratibu wa sera na mipango ya maendeleo ya rasilimaliwatu; Kushirikiana katika kuandaa mipango ya elimu na mafunzo kwa ajili ya

watu na vikundi vyenye mahitaji maalumu; Kuoanisha mitaala, vyeti na utambuzi rasmi wa taasisi za elimu na

mafunzo; Kuimarisha utafiti wa pamoja na kubaini na kuendeleza vituo vya

kuendeleza umahiri katika elimu na mafunzo; Kuimarisha shughuli za Baraza la Pamoja la Vyuo Vikuu vya Afrika

Mashariki (Inter - University Council of East Africa); na Kushirikiana katika kutoa mafunzo kwenye nyanja mbalimbali za sayansi

na teknolojia kwa kutumia taasisi zilizopo na zitakazoanzishwa.vii) Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inasisitiza kuwa na jamii:- Iliyoelimika kwa kiwango cha juu na yenye kuendelea kujifunza; Yenye msukumo wa kujitegemea; Yenye mtazamo chanya wa utamaduni wa maendeleo; na yenye kiwango cha juu cha elimu bora kwa ngazi zote.viii) Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania

unaosisitiza kuinua ubora wa maisha kwa:- Kuongeza uandikishaji katika ngazi zote za elimu na mafunzo; Kutoa elimu bora ya msingi na sekondari kwa usawa; Kupanua elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi; na elimu ya juu; na Kutoa kisomo chenye manufaa kwa wanaume na wanawake wote.

Ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza na kuweza kutekeleza malengo ya mikataba mbalimbali ya kikanda, kimataifa na kuzingatia maoni ya wadau, Sera za Elimu na Mafunzo zimepitiwa upya ili kupata sera ya elimu

17

Page 27: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

na mafunzo inayojitosheleza na inakayokwenda sambamba na mabadiliko yaliyotokea na yanayoendelea kutokea.

18

Page 28: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA 4

4.0 FALSAFA, DIRA, DHIMA NA MADHUMUNI YA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO

4.1 Falsafa ya Elimu na Mafunzo

Msingi wa elimu na mafunzo umejikita katika kumwezesha binadamu kujitegemea. Elimu inayotolewa nchini inafuata misingi ya Falsafa ya Elimu ya Kujitegemea ya mwaka 1967. Misingi hiyo ni ujifunzaji wenye manufaa (meaningful learning) katika nyanja zote kuu tatu: utambuzi, utendaji na uelekeo. Ujifunzaji wa aina hii unatambulishwa na viashiria vifuatavyo: Ushirikishaji, Uhusishaji wa Nadharia na Vitendo, Uadilifu, Kujiamini, Kujiendeleza, Kuwa na Stadi za Maisha, Ushindani, Kuthamini Usawa, Ujasiriamali, Ubunifu, Udadisi, Uvumbuzi, Uwezo wa Kuchambua na Kutathmini.

Utoaji wa elimu na mafunzo nchini utaendelea kuzingatia misingi ya Falsafa ya Elimu ya Kujitegemea kulingana na mabadiliko yanayotokea katika jamii kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi, na kiteknolojia.

4.2 Dira Sera ya elimu na mafunzo inadhamiria kuwa na:“Mtanzania aliyeelimika kwa kiwango cha juu, mwenye maarifa, stadi na mwelekeo; mahiri na aliye tayari kukabiliana na changamoto za kisiasa, kijamii na kiuchumi, kiteknolojia na kushiriki kwa ufanisi katika kufikia malengo ya maendeleo yaliyowekwa kitaifa na kimataifa”.

4.3 Dhima Kutoa fursa ya elimu na mafunzo bora kwa usawa na kuhakikisha kuwepo kwa mazingira yanayokidhi mahitaji kiutendaji kwa wadau wote wa elimu na mafunzo ili waweze kushiriki katika kutoa elimu hiyo katika ngazi zote.

19

Page 29: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

4.4 Madhumuni ya Jumla ya Sera ya Elimu na Mafunzo Kuelekeza juu ya utoaji wa elimu na mafunzo unaoendana na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiteknolojia pamoja na mahitaji ya soko la ajira, ili kuinua ubora wa maisha ya Mtanzania.

4.5 Madhumuni MahsusiSera ya elimu na mafunzo itakuwa na madhumuni mahsusi yafuatayo:a) Kuweka mfumo na muundo wa elimu na mafunzo unaotoa fursa kwa

usawa wa kijinsia kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya watu wenye ulemavu, wenye vipaji na vipawa.

b) Kuandaa na kuendeleza rasilimaliwatu katika viwango mbalimbali vitakavyokidhi mahitaji ya jamii.

c) Kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi katika utoaji wa elimu na mafunzo.

d) Kushirikisha taasisi na asasi zisizo za serikali katika utoaji wa elimu na mafunzo.

e) Kuwa na mitaala inayozingatia nadharia na vitendo katika elimu za jamii, sayansi, ufundi, teknolojia pamoja na matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kukidhi mahitaji ya taifa na kimataifa.

f) Kupanua wigo wa ugharimiaji wa elimu katika ngazi zote za elimu na mafunzo kwa kushirikisha wadau wote.

g) Kuinua ubora wa utunzaji wa mazingira kwa kutoa elimu ya mazingira katika ngazi zote za elimu.

h) Kuwa na muundo wa kisheria utakaoelekeza utoaji wa elimu na mafunzo.

i) Kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa elimu na mafunzo kati ya nchi wanachama kikanda na kimataifa.

j) Kuwa na jamii ya wanafunzi na wafanyakazi wa sekta ya elimu na mafunzo wenye stadi za kujikinga na maradhi na maambukizi ya VVU

20

Page 30: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

na UKIMWI, uwezo wa kutoa huduma na faraja kwa watu wanaoishi na VVU/ UKIMWI, walioathirika na matumizi mabaya ya dawa za kulevya; na walioathiriwa na majanga hayo.

k) Kuimarisha maarifa na kujenga stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu ili kujenga utamaduni wa kujisomea.

l) Kuimarisha uratibu na mawasiliano kati ya wizara zinazotekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo.

m) Kuwa na mfumo thabiti wa sifa linganifu kwa kila ngazi na kati ya ngazi za elimu na mafunzo inayoruhusu uhuru wa mwingiliano wa kupata sifa stahiki katika ngazi mbalimbali.

21

Page 31: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA YA 5

5.0 HOJA ZA SERA NA MATAMKO

5.1 Mfumo na Muundo wa Elimu na Mafunzo Jukumu la utoaji wa Elimu na mafunzo nchini ni la wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo. Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa husimamia na kuendesha shule za msingi na sekondari. Wizara nyingine husimamia na kuendesha mafunzo ya kisekta katika vyuo vilivyo chini ya Wizara zao. Aidha, mashirika yasiyo ya serikali na watu binafsi hutoa elimu kwa mfumo rasmi na usio rasmi kwa uratibu wa Serikali.

SualaUoanishaji wa ngazi mbalimbali katika utoaji wa Elimu na Mafunzo.

Maelezo Utaratibu wa kuendesha elimu na mafunzo hauoanishi kikamilifu shughuli za kielimu baina ya wizara na wizara, wizara na taasisi mbalimbali na taasisi na taasisi. Wizara, taasisi na mamlaka zilizopo zina mamlaka kamili ya kisheria ya kutekeleza masuala yaliyoainishwa katika sheria inayohusika hususan; mitaala, mitihani na tuzo za vyeti bila kuwa na uratibu wa pamoja. Hali hii inasababisha tofauti kati ya ubora wa elimu inayotolewa na vyombo mbalimbali na katika ulinganifu wa tuzo zinazotolewa. Aidha, kukosekana kwa uratibu thabiti na muunganiko yakinifu wa ngazi moja hadi nyingine kunapunguza ufanisi katika mfumo wa elimu. Kutokana na hali hiyo kuna umuhimu wa kuimarisha uratibu baina ya Wizara, Taasisi na Mashirika mbalimbali ili kuwepo uoanishaji wa viwango vya elimu vinavyotolewa na kuongeza njia za utoaji wa elimu na stadi mbalimbali ili wahitimu wawe na ujuzi wa kukabili mazingira. MadhumuniKuwa na tija na ufanisi katika utoaji wa elimu na mafunzo nchini.

22

Page 32: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Tamko

5.1.1 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha mfumo wa elimu na mafunzo ili kukabiliana na changamoto na mabadiliko ya kiuchumi, kisayansi na teknolojia na mahitaji ya kijamii.

5.1.2 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaboresha muundo wa elimu na mafunzo kwa kuoanisha ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo kulingana na mahitaji ya kijamii

5.2 Mfumo Rasmi wa Elimu na MafunzoMfumo huu ni wa kitaaluma na kitaalamu unaoanzia ngazi ya Elimu ya Msingi hadi elimu ya juu.

SualaMuundo wa elimu na mafunzo

Maelezo Tafiti zimeonesha kuwa nchi mbalimbali hutumia muundo kama 6-3-2-3+ na 8-4-4+. Miundo hii ina faida za kumwezesha mwanafunzi kuhitimu mapema na kutoa mchango kwa jamii kwa muda mrefu zaidi, gharama za kumsomesha mwanafunzi kwa mzazi na Serikali ni ndogo ukilinganisha na muundo unaochukua muda mrefu kwa mwanafunzi kukamilisha mzunguko wa elimu. Katika baadhi ya nchi za SADC elimu ya msingi hutolewa kwa muda wa miaka 6, hali inayopunguza gharama za kumsomesha mtoto ngazi ya msingi na kuongeza ufanisi katika mfumo wa elimu. Muundo wa elimu uliopo wa 2-7-4-2-3+ una jumla ya miaka kumi na nane kuukamilisha. Katika muundo huu mwanafunzi anakaa muda mrefu shuleni, anachelewa kutoa mchango wake kwa taifa na gharama za kumsomesha ni kubwa. Muda huu ungeweza kupungua ikiwa elimu ya awali itatolewa kwa ufanisi kwa watoto

23

Page 33: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

wote, kuondoa marudio na kupunguza mada katika mitaala ya elimu ya msingi. Hali hii itachangia kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu na mafunzo.

Mhitimu wa elimu ya msingi ana umri mdogo na maarifa na stadi za kiwango kidogo ambacho hakimwezeshi kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa kazi. Aidha, makubaliano ya mbalimbali ya haki za mtoto yanazuia ajira kwa mtoto na sera ya utumishi wa umma imeweka kiwango cha chini cha elimu na mafunzo kuingia katika utumishi wa umma kuwa ni kidato cha nne.

Kuna umuhimu wa kupunguza muda wa elimu ya awali na msingi ili rasilimali zilizopo zitumike kwa tija na ufanisi katika utoaji wa elimu ya awali, msingi na sekondari ngazi ya kawaida kwa watoto wote.

MadhumuniKuwa na mfumo wenye tija na fanisi katika utoaji wa elimu na mafunzo.

Tamko

5.2.1 Muundo wa elimu na mafunzo rasmi wa kitaaluma utakuwa 1-6-4-2-3+ yaani, mwaka mmoja wa elimu ya awali, miaka 6 ya elimu ya msingi, miaka 4 ya sekondari ngazi ya kawaida, miaka 2 ya ngazi ya juu ya sekondari na kiwango cha miaka isiyopungua 3 ya elimu ya juu.

5.2.2 Muundo wa elimu na mafunzo rasmi wa kitaalamu utakuwa 1-6-4-1+ yaani, mwaka mmoja wa elimu ya awali, miaka 6 ya elimu ya msingi, miaka 4 ya sekondari ngazi ya kawaida, mwaka 1 au zaidi wa ngazi ya elimu ya ufundi na mafunzo.

5.2.3 Elimu ya Msingi na Sekondari ngazi ya kawaida itakuwa ni ya lazima na kwa wote.

24

Page 34: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Elimu katika Vituo vya kulelea Watoto wadogo

Elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogo hutolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5. Mahitaji ya watoto hawa ni mengi na yanahitaji mazingira rafiki yatakayowawezesha kuwa na maendeleo bora kimwili, kiakili na mwelekeo na kuendelea kujifunza kwa urahisi. Mahitaji ya watoto ni pamoja na lishe bora, malezi bora, afya bora na michezo. Kwa hiyo, jukumu la kutoa elimu hiyo ni la wadau wote wa elimu na mafunzo.

SualaMazingira ya kutolea Elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogo.

Maelezo Watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5) wanahudumiwa na Wizara yenye dhamana ya maendeleo ya watoto na yenye dhamana ya Afya na Ustawi wa Jamii. Elimu inayotolewa kwa watoto hawa haina uratibu thabiti. Vituo vingi vinavyotoa Elimu hiyo haviko kwenye hali stahili ya kujenga utamaduni wa elimu na kuweka misingi bora ya elimu. Aidha, Elimu hiyo imekuwa ikitolewa pasipo vituo husika kutambuliwa na kuratibiwa rasmi, na hivyo kukosa udhibiti wa mazingira ya kutolea elimu hiyo. Miundombinu ya utoaji wa elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogo imekuwa haitoshelezi na siyo rafiki kwa walengwa. Ikumbukwe kuwa katika umri huu mtoto anahitaji malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto chini ya uangalizi wa mzazi au mlezi. Hivyo, kuna umuhimu wa kutokuwepo na vituo vya kulala isipokuwa kwa watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi. Ili kuwezesha utoaji wa elimu bora na kuleta muunganiko katika ngazi mbalimbali za elimu, inabidi elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogo itambuliwe rasmi na kuratibiwa.

MadhumuniKuwa na misingi imara ya elimu na mafunzo kwa watoto ili kubainisha vipaji

25

Page 35: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

na vipawa, na kukuza uwezo wao kimwili, kiakili na kimaadili.

Tamko

5.2.4 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha Elimu inayotolewa katika vituo vya kulelea watoto wadogo inatambuliwa rasmi na kuratibiwa.

5.2.5 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha watoto walioko katika vituo vya kulelea watoto wadogo wanapewa huduma na elimu bora.

5.2.6 Serikali itaweka utaratibu wa kuwatambua watoto wenye ulemavu, vipaji, vipawa na mahitaji mengine maalumu katika vituo vya kulelea watoto wadogo ili waweze kuendelezwa katika ngazi za juu za elimu na mafunzo.

5.2.7 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwa Vituo vya kulelea watoto wadogo ni vya kutwa tu isipokuwa makao ya watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi.

Elimu ya Awali Hivi sasa elimu ya awali ni miaka miwili kwa watoto wa umri wa miaka 5 hadi 6. Uzoefu unaonesha kuwa elimu hii inaweza kutolewa kwa ufanisi kwa muda wa mwaka mmoja ili mradi programu za elimu hii zimeandaliwa na kutolewa kwa ufanisi.

SualaUtoaji wa Elimu ya Awali.

Maelezo

26

Page 36: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Elimu ya Awali inatolewa kwa watoto wenye umri wa miaka 5 kwa muda wa miaka miwili (2). Kipindi cha miaka miwili kinamchelewesha mtoto kuanza elimu ya Msingi kwa kuwa mtoto wa miaka sita (6) ana utayari wa kuanza elimu ya msingi endapo ataandaliwa ipasavyo.

MadhumuniKuwa na mfumo fanisi katika utoaji wa Elimu ya Awali.

Tamko

5.2.8 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha watoto wote wenye umri wa miaka mitano (5) wanapata elimu bora ya Awali kwa kipindi cha mwaka mmoja (1).

5.2.9 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itahakikisha kuwa watoto walioko kwenye madarasa ya elimu ya awali wanasoma kwa utaratibu wa kutwa na wanapata huduma muhimu zikiwemo za afya na chakula bora.

5.2.10 Serikali itaweka utaratibu wa kuwatambua watoto wenye ulemavu, vipaji, vipawa na mahitaji mengine maalumu katika madarasa ya Elimu ya Awali ili waweze kuendelezwa katika ngazi za juu za elimu na mafunzo.

Elimu ya MsingiElimu ya Msingi inatolewa kwa miaka saba (7) na ni ya lazima kwa uandikishaji na mahudhurio kwa mujibu wa sheria. Madhumuni makubwa ya elimu ya msingi ni kujenga misingi ya kielimu, kijamii na kiutamaduni. Elimu hii inakusudiwa kumwezesha kila mtoto kupata maarifa, mwelekeo, ujuzi na stadi za msingi za kusoma, kuandika, kuhesabu, kubaini na kutambua changamoto zilizopo katika mazingira na mbinu za kukabiliana nazo.

Uandikishaji katika shule za msingi mwaka 2009 unaonesha kuwa asilimia

27

Page 37: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

95.9 ya watoto wa rika lengwa waliandikishwa katika shule za msingi. Takwimu hizi zinaonesha mafanikio ya kufikia elimu ya msingi kwa wote katika miaka ya hivi karibuni, endapo jitihada za kuhimiza uandikishaji katika umri unaostahili zitaendelezwa.

SualaUfanisi katika kutoa Elimu bora ya Msingi kwa wote.Maelezo Madhumuni makuu ya Elimu ya Msingi ni kumpa mtoto Elimu na Stadi bora mapema itakayokuwa msingi wa Elimu na Mafunzo katika ngazi za juu na kumuandaa kuingia katika ulimwengu wa kazi. Umri wa kuanza Elimu ya Msingi kwa sasa ni miaka saba (7). Katika umri huu mtoto anakuwa amechelewa kupata Elimu ya Msingi ambayo angeweza kuipata mapema zaidi. Kuchelewa huku kunamfanya mtoto aingie kwenye umri wenye vishawishi vingi ambavyo vinaweza kusababishia kutoandikishwa shule au kukatisha masomo kama vile ajira za utotoni na ujauzito. Aidha, kwa kuwa uzoefu unaonesha mtoto wa umri wa miaka 6 anamudu elimu ya msingi, kuna umuhimu wa kupunguza umri wa kuanza elimu hiyo ili kuongeza ufanisi katika mfumo mzima wa elimu.

MadhumuniKutoa Elimu ya Msingi kwa wote na kwa ufanisi.

Tamko

28

Page 38: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.2.11 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa miaka sita (6) wanapata Elimu ya Msingi kwa miaka sita (6).

5.2.12 Elimu ya Msingi itakuwa ni haki kwa wote; na ya lazima kwa watoto wote waliofikia umri wa miaka sita (6).

5.2.13 Serikali itaendelea kuhamasisha uanzishaji, umiliki na uendeshaji wa shule za serikali na zisizo za serikali.

5.2.14 Serikali itaweka utaratibu wa kuwatambua watoto wenye ulemavu, vipaji, vipawa na mahitaji mengine maalumu katika madarasa ya Elimu ya Msingi ili waweze kuendelezwa katika ngazi za juu za elimu na mafunzo.

SualaKubaini na kuendeleza vipawa na vipaji vya watoto kulingana na uwezo wao.

Maelezo Mfumo wa elimu uliopo unatoa nafasi ya mtoto kupata elimu ya awali, msingi na sekondari kwa ujumla bila kuzingatia mahitaji na vipaji alivyo navyo. Utaratibu uliopo huwafikiria wale wenye ufaulu wa juu wa mitihani kuwa ndio pekee wenye vipaji. Hali hii haitoi fursa ya kubaini, kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto katika umri mdogo na hivyo kupoteza rasilimaliwatu muhimu kwa maendeleo ya taifa. Aidha, hakuna utaratibu wa kuwabaini na kuwawezesha wanafunzi wenye ulemavu na wenye matatizo ya kujifunza kupata elimu stahiki. Kuna umuhimu wa kubaini na kuwaendeleza watoto wote kulingana na mahitaji yao.

MadhumuniKuwabaini na kuwaendeleza watoto wenye ulemavu, vipawa, vipaji na mahitaji mengine maalumu.

29

Page 39: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Tamko

5.2.15 Serikali itaweka utaratibu wa kuwatambua watoto wenye ulemavu, matatizo ya kujifunza na wenye vipawa na kuwapa fursa ya kupata elimu ya Msingi kulingana na uwezo wao.

Elimu ya SekondariElimu ya sekondari hutolewa kwa wanafunzi ambao wamehitimu elimu ya msingi. Elimu rasmi ya sekondari ina ngazi mbili: elimu ya sekondari ya Kawaida ya miaka minne; na elimu ya sekondari ya Juu ya miaka miwili. Ngazi ya Kawaida huanzia Kidato cha 1 hadi 4, na ya Juu ni ya Kidato cha 5 na 6. Madhumuni makubwa ya elimu ya sekondari ni kutoa nafasi ya kupata ujuzi yaani maarifa, stadi na mwelekeo ili wahitimu wajiunge na taasisi za mafunzo ya kitaalamu ya elimu ya juu.

SualaNafasi za kujiendeleza kitaaluma na kukuza ujuzi wa Stadi za Kazi na za maisha kwa watoto wanaomaliza Elimu ya Msingi.

Maelezo Ongezeko la wahitimu wa Elimu ya Msingi limesababisha mahitaji makubwa ya nafasi katika Shule za Sekondari. Vivyo hivyo, kupanuka kwa sekta rasmi na isiyo rasmi kumeongeza shughuli za kiuchumi zinazohitaji rasilimaliwatu iliyopata mafunzo bora kitaaluma na kiufundi. Ingawa serikali imetilia mkazo ujenzi wa shule za sekondari, bado shule zilizopo hazitoshi kuchukua wanafunzi wote waliohitimu elimu ya msingi. Mwaka 2008 asilimia 51.6 ya wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi walijiunga na Elimu ya sekondari mwaka 2009. Kuna umuhimu wa kurekebisha hali hii ili kuongeza nafasi za kujiendeleza na kupata rasilimaliwatu inayokidhi soko la ajira.

Madhumuni

30

Page 40: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Kuwa na mfumo wa Elimu ya Sekondari utakaowezesha wahitimu wa elimu ya sekondari kupata maarifa na stadi mbalimbali za kazi na za maisha na kuendelea na elimu ya ngazi ya juu.

Tamko

5.2.16 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwa watoto wote wanaohitimu elimu ya msingi wanapata Elimu ya Sekondari ngazi ya kawaida kwa miaka minne (4).

5.2.17 Serikali itaimarisha utaratibu wa utoaji wa elimu ya sekondari ili kuwezesha wanafunzi kupata maarifa na stadi mbalimbali za kitaaluma na kitaalamu katika ngazi hii ya elimu na mafunzo.

5.2.18 Serikali itahakikisha kuwa wanafunzi wanaosajiliwa katika elimu ya sekondari kwenye mfumo rasmi wanakamilisha mzunguko huo wa elimu.

5.2.19 Serikali itaweka utaratibu wa kuwatambua watoto wenye ulemavu, vipaji, vipawa na mahitaji mengine maalumu katika madarasa ya Elimu ya sekondari ili waweze kuendelezwa katika ngazi za juu za elimu na mafunzo.

Upangaji wa wanafunzi Kidato cha 1 na uchaguzi wa wanafunzi Kidato cha 5

SualaKujiunga na kidato cha 1 na cha 5.

MaelezoWanafunzi wanaosajiliwa katika kidato cha 1 wanatakiwa wawe wamehitimu elimu ya msingi na kufaulu kwa kiwango kilichowekwa na serikali. Baadhi ya shule zisizo za serikali husajili wanafunzi wa kidato cha 1 kwa kutumia

31

Page 41: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

mitihani ya ndani tu bila kurejea maendeleo ya wanafunzi katika mzunguko huo wa elimu. Aidha, hali hii inapunguza usahihi katika upangaji wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi na kujiunga na elimu ya sekondari. Kuna umuhimu wa kuwa na vigezo na viwango stahili vya kupanga na kuchagua wanafunzi kujiunga na ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo

MadhumuniKuwa na vigezo stahili vya kupanga na kuchagua wanafunzi wa kujiunga na ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.

Tamko

5.2.20 Upangaji wa wanafunzi kujiunga na kidato cha 1 katika shule za sekondari za serikali na zisizo za serikali utafanywa kwa kutumia matokeo ya upimaji wa maendeleo ya wanafunzi katika mzunguko huo wa elimu.

5.2.21 Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na elimu ya sekondari ya ngazi ya Juu au elimu ya ufundi na mafunzo utazingatia maendeleo ya kila siku ya mwanafunzi na ufaulu katika mtihani wa kidato cha nne (4).

Elimu ya Ualimu Elimu ya Ualimu ipo katika ngazi ya tatu ya Mfumo wa Elimu na Mafunzo. Elimu hii hutolewa katika Vyuo vya Ualimu na baadhi ya Vyuo Vikuu ambavyo husimamiwa na Serikali na Sekta binafsi.

Baadhi ya vyuo vikuu hutoa elimu ya ualimu ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahada, Stashahada na Shahada ya Uzamili. Baadhi ya walimu wa Elimu ya Ufundi Stadi huandaliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Vocational Education and Training Authority – VETA) katika chuo cha mafunzo ya Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro kwa ajili ya kufundisha katika

32

Page 42: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

vyuo vya ufundi stadi. Vyuo vya Ualimu hutoa vyeti na stashahada za elimu ya ualimu.

SualaMafunzo ya Ualimu.

Maelezo Mahitaji ya walimu kwa ngazi zote za elimu ni makubwa na yanaendelea kuongezeka. Kutokana na mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kiteknolojia duniani kuna umuhimu wa kuogeza nafasi za ualimu na kufanya marekebisho katika programu za kitaaluma na kitaalamu ili walimu wawe na uwezo wa kufundisha kwa ufanisi zaidi.

MadhumuniKuwa na walimu bora wanaotosheleza, wenye stadi stahili za ualimu.

Tamko

5.2.22 Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali vitaendelea kutoa elimu ya Ualimu kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na miongozo itolewayo na wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo.

5.2.23 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kupanua na kuboresha miundombinu ya mafunzo ya ualimu kukidhi mahitaji ya taifa.

5.2.24 Serikali itaruhusu uanzishwaji na umiliki wa asasi binafsi za mafunzo ya walimu wa elimu ya ufundi na mafunzo.

5.2.25 Serikali itaimarisha utoaji wa mafunzo ya walimu wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.

33

Page 43: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Mafunzo KaziniSualaMafunzo ya walimu kazini.

MaelezoUwezo wa walimu wa kufundisha kwa ufanisi na kukabiliana na mabadiliko yanayotokea katika mitaala hutegemea, kwa kiasi kikubwa, mafunzo kazini. Mafunzo haya ni pamoja na kabilishi, rejeshi na mafunzo mengine kazini. Mafunzo haya humwezesha mwalimu kuoanisha mafunzo ya chuoni na mahitaji halisi ya kazi ili aweze kwenda na mabadiliko yanayotokea katika taaluma na utaalamu wake. Kwa muda mrefu hakujawa na mpango endelevu wa kutoa mafunzo ya aina hizo. Upanuzi wa Elimu ya Ualimu hauna budi kwenda sambamba na programu za kuwaendeleza walimu.

MadhumuniKuwa na Mafunzo endelevu ya walimu kazini.

Tamko

5.2.26 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaweka utaratibu endelevu wa Mafunzo ya walimu kazini.

5.2.27 Mafunzo kabilishi na rejeshi kwa walimu yatakuwa ya lazima ili kuhakikisha ubora wa elimu ya ualimu.

Elimu ya Ufundi na Mafunzo Elimu ya Ufundi na Mafunzo inajumuisha Elimu na Mafunzo ya aina zote za Stadi yanayotolewa baada ya Elimu ya Sekondari katika vyuo mbalimbali ambavyo vipo chini ya Wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo, Sekta binafsi na Wizara nyingine nchini. Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi hutolewa na vyuo vya ufundi stadi vya Serikali, visivyo vya Serikali na baadhi ya shule za sekondari katika fani mbalimbali za ufundi stadi. Aidha, ngazi ya

34

Page 44: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

ufundi sanifu na uhandisi/ uteknolojia hutolewa na wizara na taasisi za Serikali na zisizo za Serikali.

SualaUtoaji fanisi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

Maelezo Elimu ya Ufundi na Mafunzo inatolewa katika ngazi ya ufundi stadi, sanifu na uhandisi/uteknolojia. Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Vocational Education and Training Authority – VETA) husimamia ubora wa mafunzo yatolewayo ngazi ya ufundi stadi. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education – NACTE) husimamia mafunzo ya elimu ya ufundi ngazi ya ufundi sanifu na uhandisi/ uteknolojia.

MadhumuniKuwa na uratibu endelevu wa utoaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo katika Muundo wa Elimu na Mafunzo.

Tamko

35

Page 45: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.2.28 Serikali itaimarisha utaratibu wa kuvitambua rasmi na kuviratibu Vyuo vya serikali na visivyo vya Serikali vinavyotoa Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

5.2.29 Serikali itaweka utaratibu utakaowezesha wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina yao katika kutoa elimu na mafunzo endelevu.

5.2.30 Serikali itaimarisha Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kuanzisha mkondo wa pili wa Elimu ya Sekondari utakaowawezesha wahitimu wa elimu ya Msingi kusoma baadhi ya masomo ya Sekondari na Masomo ya Ufundi. Mkondo huu utakuwa pia na madarasa ya kuwaendeleza mafundi walioko kazini.

SualaMafunzo ya Wakufunzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

Maelezo Mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika katika Mfumo na Muundo wa Elimu katika ngazi ya Msingi, Sekondari na Ufundi yameongeza mahitaji ya wakufunzi na walimu wa kufundisha stadi mbalimbali. Aidha, idadi ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo imekuwa ikiongezeka kwa kasi kubwa na kusababisha ongezeko la mahitaji ya wakufunzi mwaka hadi mwaka katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Kwa sasa kipo chuo kimoja tu kinachotoa wakufunzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ambacho hakikidhi mahitaji ya kitaifa. Aidha, hakuna maandalizi rasmi ya wakufunzi wa vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo katika ngazi zote. Kwa sasa kuna walimu wengi wanaofundisha masomo ya kitaalamu katika vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ngazi mbalimbali ambao hawajapata mafunzo ya ualimu

Ongezeko la mahitaji ya wakufunzi wa Elimu ya ufundi na Mafunzo

36

Page 46: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

linachagizwa na baadhi ya wakufunzi kuhama kufuata ajira zenye kipato kizuri zaidi nje ya Mfumo wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo. Kuna umuhimu wa kupanua upatikanaji wa wakufunzi na kuwabakiza kazini.

MadhumuniKuwa na Wakufunzi bora na wa kutosha kukidhi mahitaji ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

Tamko

5.2.31 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itapanua utoaji wa mafunzo ya wakufunzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo katika ngazi zote.

5.2.32 Serikali itaimarisha uratibu na ushirikishaji wa sekta binafsi katika utoaji wa wakufunzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

5.2.33 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaweka mazingira yatakayowavutia wakufunzi na walimu kubaki kazini.

5.2.34 Serikali itaweka utaratibu wa kupata wakufunzi wa elimu ya ufundi wenye uzoefu, taaluma stahiki ya fani husika na utaalamu wa ualimu.

SualaUpatikanaji wa wataalamu wa ngazi za ufundi sanifu na uhandisi/ uteknolojia wa elimu ya ufundi na mafunzo

Maelezo Ngazi ya ufundi sanifu ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo haitoi wahitimu wa kutosha wenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira. Wataalamu wa ngazi hii wanatakiwa sio tu katika sekta za uzalishaji na huduma, bali pia katika kutoa Elimu ya Ufundi na Mafunzo. Aidha, vyuo vilivyopo havitoi wataalamu wa kutosheleza mahitaji, hivyo kuna umuhimu wa kuongeza uwezo wa kutoa

37

Page 47: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

wataalamu kwenye fani mbalimbali za Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

MadhumuniKuwa na wataalamu wa Ufundi Sanifu wenye Elimu ya Ufundi na Ujuzi wa fani mbalimbali wanaokidhi mahitaji.

Tamko

5.2.35 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaimarisha Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya ufundi Stadi vya mikoa ili kuweza kutoa mafunzo ya ngazi mbalimbali za elimu ya ufundi na mafunzo.

5.2.36 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itawezesha Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo kutoa Mafunzo ya fani na stadi mbalimbali kwa pamoja ili kupanua uwezo wa utoaji wa wahitimu wa ngazi ya Ufundi sanifu na Uhandisi / Uteknolojia.

5.2.37 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaimarisha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kwa lengo la kuongeza utoaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

5.2.38 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itapanua na kuimarisha Elimu ya Ufundi na Mafunzo katika ngazi ya ufundi sanifu na uhandisi/ uteknolojia.

Elimu ya JuuElimu ya Juu hutolewa baada ya Elimu ya Sekondari kwa lengo la kupata rasilimaliwatu wenye taaluma na utaalamu katika fani mbalimbali. Elimu hii hutolewa katika vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo na vyuo vikuu vya serikali na visivyo vya serikali katika mfumo rasmi na nje ya mfumo rasmi.

Suala

38

Page 48: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Upatikanaji wa wataalamu wenye Elimu ya Juu.

Maelezo Udahili wa wanafunzi wa rika lengwa katika vyuo vya Elimu ya Juu nchini ni mdogo kwa sababu ya uwezo mdogo wa vyuo hivyo, ingawaje ni vingi. Aidha, uendeshaji wake ni wa gharama kubwa na miundombinu yake haitoshelezi mahitaji ya makundi na fani mbalimbali. Hali hii inasababisha baadhi ya wahitimu kutokuwa na stadi zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira. Kwa hali hiyo kuna umuhimu wa kuongeza nafasi za Elimu ya Juu.

MadhumuniKuwa na wataalamu wanaokidhi mahitaji ya jamii.

Tamko

5.2.39 Serikali itarekebisha matumizi na mahitaji (rationalize) ya vyuo vya Elimu ya Juu ili kuongeza tija na ufanisi wa utoaji wa Elimu ya Juu.

5.2.40 Serikali kwa kushirikiana na wadau itapanua nafasi za Elimu ya Juu kwa jinsi zote, watu wenye ulemavu na wanaoishi katika mazingira magumu.

Suala Wataalamu wenye Elimu ya Uzamili na Uzamivu

Maelezo Sekta za uzalishaji na huduma zinahitaji wataalamu wenye elimu ya uzamili na uzamivu. Aidha, Vyuo vya Elimu ya Juu vinahitaji wahadhiri wenye kiwango cha elimu ya uzamili na uzamivu. Mahitaji katika maeneo haya yanaongezeka mwaka hadi mwaka. Ongezeko la mahitaji haya haliendani na ongezeko la udahili katika mafunzo ya Uzamili na Uzamivu. Licha ya udahili

39

Page 49: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

mdogo, programu za shahada za juu zinachukua muda mrefu kwa wanachuo kuhitimu na hivyo kutowavutia wanachuo wengi wenye sifa kujiunga na programu hizo. Hali hii inasababisha upungufu wa wataalamu wenye sifa hizo katika sekta mbalimbali.

MadhumuniKuwa na wataalamu wenye elimu ya Uzamili na Uzamivu wanaokidhi mahitaji.

Tamko

5.2.41 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaweka utaratibu wa ufadhili kwa Mafunzo ya Uzamili na Uzamivu kulingana na vipaumbele vya taifa.

5.2.42 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaongeza nafasi za Mafunzo ya Uzamili na Uzamivu na kuhakikisha uendeshaji wa programu za shahada za juu unafanyika kwa ufanisi.

5.2.43 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaweka mazingira ya kuviwezesha vyuo vya Elimu ya Juu viwe na utendaji uliotukuka na kutambulika kama vituo mahiri (Centres of Excellence)

SualaKubakiza wakufunzi na wahadhiri katika ajira zao.

MaelezoVyuo vya Elimu ya Juu vinapoteza wakufunzi na wahadhiri ambao wanahama kwenda sehemu zenye maslahi mazuri zaidi na kusababisha upungufu mkubwa wa wahadhiri, hususan katika fani za Hisabati, Sayansi na Lugha. Miundombinu isiyokidhi mahitaji na maslahi duni ya Wakufunzi na Wahadhiri hayawavutii kubaki katika ajira zao. Kwa hiyo, ni muhimu kuweka mazingira

40

Page 50: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

bora ya ajira na kazi ili kuwapata na kuwabakiza wataalamu wenye sifa stahili.

MadhumuniKuwa na Wakufunzi na Wahadhiri wa fani mbalimbali wa kutosheleza mahitaji.

Tamko

5.2.44 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaweka mazingira ya ajira na kazi yanayovutia Wakufunzi na Wahadhiri kubaki katika ajira.

SualaProgramu za Mafunzo ya Sayansi na Teknolojia katika vyuo vya Elimu ya juu.

Maelezo Mahitaji ya wataalamu wa Sayansi na Teknolojia ni makubwa na matumizi yake ni mengi na yanazidi kuongezeka. Katika karne hii wataalamu wa Sayansi na Teknolojia ndiyo msingi wa mageuzi makubwa ya maendeleo katika nyanja zote. Pamoja na mwelekeo huo, hakuna maoteo halisi ya mahitaji ya rasilimaliwatu kitaifa. Hali hii inafanya vyuo vya Elimu ya Juu vidahili wanafunzi bila mwongozo wa mahitaji ya kitaifa ya wataalamu wa aina mbalimbali. Hivyo, husababisha kuwepo kwa baadhi ya progamu za mafunzo yasiyolenga mahitaji ya wataalamu.

Kuna umuhimu wa kuwa na maoteo halisi ya kitaifa ya mahitaji ya rasilimaliwatu ili kufanikisha mageuzi katika matumizi ya sayansi na teknolojia kwa maendeleo ya nchi.

Madhumuni

41

Page 51: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Kuwa na programu za mafunzo zinazolenga mahitaji ya kitaifa.

Tamko

5.2.45 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaweka maoteo halisi ya kitaifa ya mahitaji ya wataalamu wa Sayansi na Teknolojia.

SualaUshirikiano wa kitaasisi na kitaaluma kati ya vyuo vya Elimu ya Juu na Taasisi za ndani na za nje.

MaelezoVyuo na Taasisi za Elimu ya Juu vinatakiwa kuwa na mawasiliano na mahusiano ili kuwezesha ulinganifu wa programu za mafunzo, kupunguza gharama za uendeshaji kwa kutumia kwa pamoja vitendea kazi na kubadilishana wanafunzi na wataalamu. Hali hii itaongeza tija na ufanisi katika utoaji wa Elimu ya Juu. Hivyo ni muhimu vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu kuimarisha ushirikiano baina yao.

MadhumuniKuwa na mawasiliano na uhusiano wa kielimu baina ya vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu ili kuleta tija na Ufanisi.

Tamko

42

Page 52: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.2.46 Serikali itaweka utaratibu utakaowezesha vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina yao kwa maslahi ya taifa.

5.2.47 Serikali itahamasisha na kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kitaasisi na kitaaluma, kitaifa na kimataifa kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

SualaMfumo wa sifa linganifu za Kitaifa na Kimataifa wa tuzo na vyeti

Maelezo Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo ngazi zote hupanga na kuendesha mafunzo na kisha kutoa tuzo na vyeti kwa ngazi husika ya elimu na mafunzo. Ili kuhakikisha kuwa tuzo na vyeti hivyo vinatambulika ndani na nje ya nchi ni muhimu kuwa na mfumo wa kitaifa wa sifa linganifu za tuzo na vyeti unaowiana na mifumo ya kimataifa. Mfumo huo utaondoa kasoro zilizopo za sifa za Elimu na Mafunzo zitolewazo nchini na nje ya nchi.

MadhumuniKuwa na Mfumo wa kitaifa wa sifa linganifu wa tuzo na vyeti unaowiana na mifumo ya kimataifa

Tamko:

5.2.48 Serikali itaweka na kusimamia mfumo wa kitaifa wa sifa linganifu wa tuzo na vyeti kwa ngazi zote za Elimu na Mafunzo (National Education Standards).

Utoaji wa Elimu na Mafunzo

Utoaji wa Elimu na mafunzo unazingatia fursa na usawa kwa rika na makundi

43

Page 53: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

yote. Hali kadhalika, unatilia mkazo ubora wa elimu na mafunzo yatolewayo ili kukidhi mahitaji ya jamii na kujenga utaifa. Ili kufanikisha uwepo wa fursa na usawa katika utoaji wa elimu na mafunzo, ni muhimu kuwa na shule na vyuo vyenye nyenzo na mazingira stahiki kukidhi uandikishaji na udahili wa makundi yote .

SualaFursa na usawa katika utoaji wa elimu na mafunzo

Maelezo Utoaji wa Elimu na Mafunzo unazingatia upatikanaji wa nafasi za elimu na mafunzo bila ubaguzi wa jinsi, rangi, kabila, dini, hali ya kijamii au kipato ili kufikia malengo ya elimu ya msingi kwa wote na kupanua nafasi kwa makundi mbalimbali. Aidha, elimu ya msingi ni haki ya kila raia. Pamoja na juhudi za Serikali za kutoa nafasi za elimu kwa makundi yote, baadhi ya makundi bado hayajafikiwa kikamilifu kutokana na sababu za kijamii, kiuchumi na kijiografia. Hali hii inasababisha kutofikiwa kwa malengo ya kitaifa na kimataifa katika maendeleo.

MadhumuniKuwa na elimu na mafunzo yanayotolewa kwa usawa.

Tamko

44

Page 54: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.2.49 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahamasisha na kuimarisha upatikanaji wa elimu na mafunzo kwa usawa.

5.2.50 Serikali itaendelea kupanua nafasi za upatikanaji wa elimu ya sekondari, elimu ya ufundi na mafunzo na Elimu ya Juu.

5.2.51 Serikali itaendelea kuhimiza na kuhakikisha msambazo wa asasi za elimu na mafunzo kwa uwiano stahili.

5.2.52 Serikali itaweka utaratibu utakaohakikisha kuwa wanafunzi wa jinsi zote, kwa usawa, wanatambuliwa, wanaandikishwa shuleni na wanahitimu elimu ya ngazi husika.

5.2.53 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaweka utaratibu wa kuinua ushiriki na ufaulu wa wanafunzi wa jinsi zote katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

Suala Utaifa katika utoaji wa elimu na mafunzo.

Maelezo Elimu ya sekondari inatolewa katika shule za bweni na za kutwa za serikali na zisizo za serikali. Shule za serikali za kutwa zilizojengwa kwa nguvu za wananchi, zinasomesha watoto wanaotoka kwenye maeneo yao zaidi kuliko maeneo mengine ya nchi. Hii inapunguza kuchanganyika kwa wanafunzi na hivyo kuleta umoja wa kikabila badala ya kuimarisha na kujenga utamaduni na uzalendo wa kitaifa. Kuchanganyika kwa wanafunzi kunawapa fursa pana zaidi ya kushirikishana uzoefu na maarifa hivyo kuongeza ufanisi wa matumizi ya vipawa na vipaji. Shule za bweni zilikuwa zinachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, kwa kutumia kigezo cha mgao maalumu kimkoa kwa ngazi ya kawaida ya elimu ya sekondari. Utaratibu huu ulikuwa na lengo la kuleta usawa katika maendeleo, na kujenga utaifa miongoni mwa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Kwa sasa wanafunzi wa kidato cha 1

45

Page 55: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

wanachaguliwa kwenda kwenye shule za sekondari za kutwa ngazi ya kata.

Katika elimu ya sekondari ngazi ya juu, wanafunzi wanachaguliwa kwa kuzingatia ufaulu na mchepuo wa masomo katika mtihani wa taifa wa kidato cha 4, kwenda shule za bweni na za kutwa zenye hosteli kote nchini. Mchanganyiko wa wanafunzi wa elimu ya sekondari ngazi ya juu huzingatia ufaulu na chaguzi za masomo. Aidha, katika shule za sekondari za bweni ngazi ya kawaida mchanganyiko ulikuwa ni wa mgao maalumu kimkoa kwa nchi nzima. Kwa hiyo kuna umuhimu wa kuimarisha shule za bweni kwa sekondari ngazi ya kawaida ili kuleta usawa wa maendeleo kielimu; kujenga na kuimarisha utaifa miongoni mwa wanafunzi na wananchi.

MadhumuniKuwa na maendeleo ya kielimu kwa usawa na kujenga utaifa.

Tamko

5.2.54 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kujenga na kupanua shule za sekondari za bweni.

5.2.55 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kuhamasisha ujenzi wa hosteli katika shule za sekondari za kutwa.

5.2.56 Serikali itaweka utaratibu wa kuwezesha shule za bweni na zenye hosteli kupokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

SualaMakundi yenye Mahitaji Maalumu ya Elimu na Mafunzo.

Maelezo Pamoja na jitihada za kutoa elimu kwa wote, baadhi ya makundi katika jamii yamekuwa hayapati elimu ipasavyo. Mengine yamekuwa hayapati haki hii

46

Page 56: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

kutokana na mtindo wao wa maisha, kwa mfano; wanaoishi kwa kuhamahama, watoto wa mitaani na wanaoishi katika mazingira magumu. Makundi mengine ni pamoja na wenye ulemavu wa aina mbalimbali. Kuna umuhimu wa kupunguza vikwazo vya kupata elimu na mafunzo kwa kuongeza rasilimali za kutoa elimu na mafunzo kwa makundi haya.

Madhumuni Kuwa na mfumo madhubuti unaopunguza vikwazo vya kupata elimu na mafunzo kwa makundi yenye mahitaji maalumu.

Tamko

5.2.57 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha utaratibu wa kutoa elimu na mafunzo kwa makundi yenye mahitaji maalumu.

SualaUsawa wa kijinsia katika mfumo wa elimu na mafunzo.

MaelezoAzma ya serikali ni kuwa na mfumo unaozingatia usawa wa kijinsia katika ngazi zote za elimu na mafunzo. Uwiano wa uandikishaji wa wavulana kwa wasichana kwa mwaka 2009 ulikuwa; 1:1 katika ngazi ya shule za msingi, 1:0.8 katika ngazi ya Sekondari ya Kawaida na 1:0.7 katika ngazi ya Sekondari ya Juu. Aidha, Udahili wa wasichana katika ngazi ya shahada ya kwanza kwa mwaka 2007 ulikuwa asilimia 31.7, asilimia 28.4 katika ngazi ya uzamili na asilimia 19.7 katika ngazi ya uzamivu. Pamoja na hayo kuna mdondoko wa wasichana na wavulana katika mfumo wa elimu kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ya ujauzito. Kati ya wasichana 38,890 walioacha shule kwa sababu mbalimbali katika ngazi ya elimu ya msingi mwaka 2008,

47

Page 57: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

3,370 waliacha kwa sababu ya ujauzito sawa na asilimia 9.9. Kati ya wasichana 22,584 walioacha shule katika elimu ya sekondari ngazi ya ya kawaida mwaka 2008, 4,941 waliacha kwa sababu ya ujauzito sawa na asilimia 21.9. Kati ya wasichana 192 walioacha shule katika ngazi ya elimu ya sekondari ya juu mwaka 2008, 24 waliacha kwa sababu ya ujauzito sawa na asilimia 6.4.

Ni dhahiri kwamba ushiriki wa wasichana katika elimu kuanzia ngazi ya elimu ya sekondari kwenda ngazi za juu ni mdogo ukilinganisha na wavulana. Hali hii inahitaji marekebisho ili kufikia usawa wa kijinsia katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

MadhumuniKuwa na usawa wa kijinsia katika mfumo wa elimu na mafunzo.

Tamko

48

Page 58: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.2.58 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahimiza ujenzi wa hosteli katika shule za sekondari za kutwa kwa ajili ya kuhamasisha ushiriki wa wasichana na wavulana katika ngazi hii ya elimu.

5.2.59 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kuhamasisha uanzishwaji wa shule za sekondari za Ngazi ya Juu kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

5.2.60 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha utaratibu wa kuhamasisha wasichana na wavulana kusoma hisabati na sayansi katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.2.61 Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa mitazamo na mawazo mgando ya ujinsi yanaondolewa katika mfumo mzima wa elimu na mafunzo.

5.2.62 Serikali itaweka utaratibu wa kuwawezesha wanafunzi wa kike wa shule wanaopata ujauzito kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

5.2.63 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwa programu za elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi zinaendelea kusisitiza ushiriki wa jinsi zote.

5.2.64 Serikali itaweka utaratibu wa kuwabaini na kuchukua hatua stahiki dhidi ya watu watakaosababisha wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari kukatisha masomo yao.

Elimu JumuishiSualaElimu jumuishi katika utoaji wa elimu na mafunzo.

MaelezoElimu jumuishi ni mfumo wa utoaji wa elimu na mafunzo unaowafanya

49

Page 59: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

wanafunzi wote wawe sehemu ya jamii moja ya shule kwa kuzingatia mahitaji yao bila ubaguzi na kwa kutumia rasilimali kikamilifu. Utaratibu huu unawafanya wanafunzi wa aina zote wajione kuwa wanakubalika na kila mmoja wao, na tofauti zao hazipaswi kuwa kikwazo cha kupata elimu na mafunzo kwa usawa. Ili kuwezesha kuwepo kwa elimu jumuishi, baadhi ya shule na vyuo vimewekewa miundombinu na vifaa na rasilimaliwatu stahiki. Hata hivyo, kutokana na gharama kubwa ya vifaa, miundombinu na rasilimaliwatu, utoaji wa elimu jumuishi nchini bado haujafikia kiwango stahiki.

Pamoja na umuhimu wa kuwa na elimu jumuishi, bado kuna umuhimu wa kuwa na utaratibu maalumu wa kuwahudumia wanafunzi wenye ulemavu wa aina tofauti ndani ya shule wasioweza kuchanganyika na wengine kwa mfano, wasiiona, viziwi, wenye otizim na wenye ulemavu wa akili.

MadhumuniKuimarisha utoaji wa elimu jumuishi nchini.

Tamko

5.2.65 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaimarisha utaratibu wa utoaji elimu jumuishi katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.2.66 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwa rasilimaliwatu, miundombinu na vifaa stahiki vinapatikana kwa ajili ya utoaji wa elimu jumuishi katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.2.67 Serikali kwa kushirikiana na wadau itawatambua na kuwahudumia wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika kujifunza.

50

Page 60: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.3 Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Elimu ya watu wazima hujumuisha utoaji wa maarifa na stadi za kusoma, kuandika, kuhesabu na kujiendeleza baada ya kupata stadi hizo kwa watu wazima.

Elimu ya watu wazima hutoa fursa kwa watu wazima kuendelea kujifunza katika muda wote wa maisha yao (Life long Learning).

Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ni elimu itolewayo kwa waliokosa kupata elimu katika ngazi mbalimbali za mfumo rasmi wa elimu na wanaohitaji kujiendeleza. Utoaji wa elimu nje ya mfumo rasmi unazingatia mahitaji ya walengwa. Aidha, programu za elimu hii zina muundo wenye mpangilio na hutumia mbinu shirikishi za kufundishia na kujifunzia.

Wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo inasimamia uandaaji wa sera ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi, huchambua na kuweka viwango vya utekelezaji wa sera hiyo, huratibu na kutathmini mipango ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi. Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inaendesha elimu kwa njia ya masafa na ana kwa ana na inatoa mafunzo ya taaluma na utaalamu wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.

Elimu ya kujiendeleza kwenye fani za ufundi stadi hutolewa na vituo vya ufundi stadi vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Halmashauri na Sekta Binafsi. Aidha, Elimu ya kujiendeleza inatolewa na vituo vya sekta binafsi kwa utaratibu wa masomo ya ziada.

Elimu ya Watu WazimaSuala

51

Page 61: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Elimu ya msingi na Elimu ya kujiendeleza kwa Watu Wazima.

MaelezoUtoaji wa elimu ya watu wazima nchini umejumuisha elimu na shughuli za jamii kupitia MUKEJA. Mazingira ya kutolea elimu watu wazima kupitia MUKEJA yanaathiriwa na miundombinu isiyovutia kwa watu wazima kushiriki katika Elimu hiyo. Aidha, hakuna wataalamu mahsusi wa kutosha na miundombinu ya kutosheleza mahitaji ya kutolea elimu hiyo. Kutokana na hali hiyo kuna umuhimu wa kuimarisha miundombinu na mbinu sahihi za kutolea Elimu hiyo na wataalamu wa kutosha kufundisha.

Elimu ya kujiendeleza haijawafikia walengwa wote katika Jamii. Hali hii inasababishwa na upungufu wa miundombinu, rasilimaliwatu, fedha na vitendea kazi. Upo umuhimu wa kuimarisha utoaji wa elimu hii kwa wote.

MadhumuniKuwa na Watu Wazima wenye stadi za kusoma, kuandika, kuhesabu (KKK) na wenye ari ya kujiendeleza.

Tamko

5.3.1 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaandaa utaratibu wa kuendeleza Elimu ya Watu Wazima (EWW) nchini.

5.3.2 Serikali kwa kushirikiana na wadau itazifanya taasisi zote za Elimu na Mafunzo nchini kuwa Vituo vya Elimu ya Watu Wazima.

Elimu Nje ya Mfumo RasmiSualaUtoaji wa Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

52

Page 62: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

MaelezoElimu Nje ya Mfumo rasmi hutolewa na Wizara, Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali na watu binafsi. Utoaji huo hufanyika bila uratibu thabiti wa kitaifa. Hali hii inasababisha kuwa na viwango visivyokidhi ubora wa elimu itolewayo.

Elimu na Mafunzo nje ya Mfumo Rasmi yanahitaji uratibu thabiti ili kuyafanya yawe na mwelekeo na muunganiko sahihi na Mfumo Rasmi.

Madhumuni Kuwa na uratibu thabiti wa utoaji wa Elimu na mafunzo nje ya Mfumo rasmi.

Tamko

5.3.3 Serikali itaweka utaratibu wa kuvitambua rasmi na kuviratibu vituo vyote vinavyotoa Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

5.3.4 Serikali itarekebisha muundo na majukumu ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ili iwe Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

5.3.5 Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi itaratibu vituo vinavyotoa Elimu kwa masafa na elimu ya kujiendeleza isipokuwa vile vyenye uratibu wa vyombo vingine vya Wizara.

5.4 Mitaala ya Elimu na Mafunzo

Mtaala wa elimu na mafunzo ni mpangilio wa malengo, maudhui na mchakato wa kufikia matarajio ya jamii na taifa katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Aidha, ni jumla ya matendo yote yaliyoratibiwa yanayofanywa katika shule na vyuo. Kwa hiyo, kila ngazi ya elimu na

53

Page 63: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

mafunzo haina budi kuwa na mtaala.

Suala Mitaala ya Shule na Vyuo

MaelezoMaudhui ya mitaala iliyopo hayatoshelezi kumwelimisha mwanafunzi aweze kupata maarifa, stadi na mwelekeo kulingana na mahitaji ya jamii na ulimwengu wa kazi. Changamoto zinazojitokeza ni katika maandalizi ya mitaala stahiki na upatikanaji wa rasilimali mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wake. Changamoto hizi zinaathiri ubora wa Elimu na Mafunzo yatolewayo. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuimarisha uandaaji na utekelezaji wa mitaala katika ngazi zote za Elimu na Mafunzo.

MadhumuniKuwa na maandalizi na utekelezaji thabiti wa mitaala katika ngazi zote za Elimu na Mafunzo.

Tamko.

54

Page 64: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.4.1 Serikali itahakikisha kuwa majukumu ya maandalizi, ukuzaji, ufuatiliaji na tathmini ya mitaala ya elimu na mafunzo katika ngazi za shule na vyuo yanaendelea kufanywa na chombo kilichopewa majukumu hayo.

5.4.2 Serikali itaweka utaratibu madhubuti wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mitaala inayozingatia umahiri wa kumudu stadi za maisha na za kazi.

5.4.3 Serikali itaweka utaratibu endelevu wa kuendesha mafunzo kabilishi na rekebishi kwa watekelezaji wa mitaala.

5.4.4 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwepo kwa miundombinu inayotosheleza mahitaji ya utekelezaji wa mitaala.

5.4.5 Serikali itaandaa mitaala inayokidhi mahitaji ya makundi yote ya wanafunzi na jamii kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa.

Elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogoSuala Mtaala wa elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogo.

MaelezoElimu inayotolewa katika vituo vya kulelea watoto wadogo haina uratibu maalumu. Aidha, miaka kati ya 3 na 4 ni miaka ambayo mtoto anajenga dhana, mwelekeo na haiba hivyo anahitaji kuwekewa misingi thabiti ya uelewa na maadili. Kuna umuhimu wa elimu inayotolewa katika vituo hivyo kuwa na stadi za msingi kulingana na umri wao. MadhumuniKuwa na elimu bora ya kumjengea mtoto stadi za msingi za elimu na

55

Page 65: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

maisha.

Tamko

5.4.6 Serikali itahakikisha mtaala wa Elimu katika vituo vya kulelea watoto wadogo unaandaliwa kukidhi mahitaji ya watoto na jamii.

Elimu ya awaliMaelezoElimu ya awali hutolewa kwa miaka 2 kwa watoto wa umri wa miaka 5 hadi 6 na huwaandaa kwa ajili ya elimu ya msingi. Mtaala katika ngazi hii hauna budi kuwa na maudhui ya msingi na stadi za kumwandaa mtoto kwa ngazi inayofuata ya elimu.

Suala Maudhui na stadi za elimu ya awali

MadhumuniKuwa na mtaala wenye maudhui ya msingi na stadi anuwai

Tamko

5.4.7 Serikali itaandaa mtaala wa elimu ya awali wenye maudhui ya msingi na stadi anuwai zinazokidhi mahitaji ya watoto na jamii.

5.4.8 Elimu na mafunzo ya maadili itakuwa ni sehemu ya mitaala katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.4.9 Elimu ya Uzalendo na Utaifa itakuwa ni sehemu ya mitaala katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

56

Page 66: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Elimu ya msingi

SualaMtaala wa Elimu ya Msingi.

Maelezo Maendeleo makubwa na ya haraka katika sayansi na teknolojia, na hasa teknolojia ya kupashana habari yamesababisha mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Hali hii imeleta changamoto katika mifumo mbalimbali ikiwemo ya elimu na mafunzo. Utekelezaji wa mtaala na upimaji wa maendeleo ya wanafunzi huegemea zaidi maarifa kuliko ujuzi na umahiri wa maudhui. Kwa hali hiyo, mtaala wa Elimu ya Msingi haukidhi mahitaji ya mhitimu katika kukabiliana na changamoto za jamii na maandalizi ya elimu na mafunzo katika ngazi za juu. Kutokana na upungufu huo, ipo haja ya kupitia upya mtaala huo ili kukidhi mahitaji.

MadhumuniKuwa na elimu bora ya Msingi itakayokidhi mahitaji ya Kiteknolojia, Kiuchumi, na Kijamii.

Tamko

5.4.10 Mtaala wa Elimu ya Msingi utahuishwa kulingana na mabadiliko ya kiteknolojia, kiuchumi na kijamii.

5.4.11 Stadi za Maisha, Stadi za Kazi, Stadi za Mawasiliano na Ujasiriamali zitafundishwa kinadharia na kwa vitendo katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.4.12 Serikali itarekebisha mtaala wa elimu ya msingi ili kuingiza maudhui ya msingi ya elimu ya ufundi.

57

Page 67: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Elimu ya SekondariSualaMtaala wa elimu ya sekondari unaotosheleza mahitaji

MaelezoLengo kuu la elimu ya sekondari ni kutoa nafasi ya kupata maarifa, stadi na mwelekeo ili wahitimu waweze kujiunga na mafunzo ya kitaaalamu na kitaaluma katika ngazi mbalimbali. Aidha, wahitimu wanaweza kuingia kwenye ulimwengu wa kazi. Mtaala wa elimu katika ngazi hii hauna budi kuzingatia mahitaji ya makundi mbalimbali ya wanafunzi, jamii na ya soko la ajira.

MadhumuniKuwa na wahitimu wa elimu ya sekondari wenye maarifa, stadi na mwelekeo wa kuendelea na elimu na mafunzo au ulimwengu wa kazi.

Tamko

5.4.13 Serikali itaandaa mtaala wa elimu ya sekondari wenye maudhui ya maarifa na stadi za Elimu ya Ufundi wa fani mbalimbli zitakazokidhi mahitaji ya jamii na soko la ajira.

Elimu ya Ualimu

SualaMtaala wa elimu ya ualimu unaotosheleza mahitaji

MaelezoProgramu za ualimu zinazotolewa katika ngazi za cheti, stashahada na shahada hazina muunganiko wa kimaudhui kutoka ngazi moja kwenda

58

Page 68: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

nyingine. Ni muhimu kuwa na mafunzo ya msingi ya elimu ya ualimu yanayotolewa kwa ngazi zote.

MadhumuniKuwa na walimu bora wanaotosheleza, wenye stadi stahili za msingi za ualimu.

Tamko

5.4.14 Serikali itaweka utaratibu wa kuwa na mafunzo ya msingi ya elimu ya ualimu kwa walimu wote na kufanya Programu za elimu ya ualimu kuwa na muunganiko wa kitaalamu kwa ngazi zote.

5.4.15 Serikali itaweka utaratibu wa kuandaa walimu utakaozingatia mahitaji ya vipaumbele vya taifa.

Taaluma ya Mkufunzi

SualaUjuzi na Taaluma ya Wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu. MaelezoWakufunzi wanaofundisha katika Vyuo vya Ualimu wana shahada za elimu za taaluma za masomo ya sayansi na sayansi jamii na wengine wana stashahada za ualimu. Hali kadhalika, baadhi yao wana shahada za sayansi na sayansi jamii na ualimu. Aidha, wapo wenye shahada za sayansi na sayansi jamii bila taaluma ya ualimu na wapo ambao hawana uzoefu wa kufundisha katika ngazi yoyote ya elimu. Hali hii inasababisha kuwa na walimu ambao hawajaandaliwa kikamilifu. Kuna umuhimu wa kuwa na wakufunzi stahiki katika vyuo vyote vya ualimu.

59

Page 69: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

MadhumuniKuwa na wakufunzi wenye sifa stahiki za kufundisha katika vyuo vya ualimu.

Tamko

5.4.16 Serikali itaweka utaratibu wa kupata wakufunzi wenye uzoefu, taaluma stahiki ya fani husika na utaalamu wa ualimu.

5.4.17 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaviwezesha Vyuo vya ualimu kuwa na vifaa na programu za mafunzo za kuwaendeleza walimu kitaaluma na kitaalamu.

Mazoezi ya Kufundisha

Suala Mafunzo kwa vitendo na mazoezi ya kufundisha kwa wanachuo.

MaelezoMazoezi ya kufundisha yanawawezesha wanachuo kutumia nadharia waliyofundishwa katika hali halisi. Mazoezi haya yanawapa wanachuo uzoefu wa kufundisha na kukabiliana na changamoto zilizopo katika mazingira halisi watakayofanyia kazi baada ya kuhitimu.

MadhumuniKuwa na mafunzo kwa vitendo na mazoezi ya kufundisha ili kuimarisha utaalamu wa walimu.

Tamko

60

Page 70: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.4.18 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha Mafunzo kwa vitendo kwenye maabara na karakana; na mazoezi ya kufundisha katika vyuo vya ualimu.

5.4.19 Serikali itahakikisha kuwa wamiliki wa vyuo vya ualimu vya serikali na visivyo vya serikali wanagharimia mafunzo kwa vitendo kwa walimu wanafunzi.

Elimu ya Ufundi na Mafunzo

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi hutayarisha mitaala kwa ajili ya mafunzo ya ufundi stadi. Aidha, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi hutoa utambuzi rasmi wa vyuo vya elimu ya ufundi na miongozo ya utayarishaji wa Programu za mafunzo yanayotolewa na vyuo hivyo. Tume ya Taifa ya Vyuo Vikuu hutoa utambuzi rasmi wa vyuo vikuu ambao unaviwezesha vyuo hivyo kuandaa programu za mafunzo ya vyuo vyao. Taasisi ya Elimu Tanzania hukuza mitaala na kuandaa mihtasari ya masomo mbalimbali kwa ngazi ya elimu ya Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu

Suala Utoshelevu wa mitaala ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo

Maelezo Mitaala ya elimu ya ufundi na mafunzo haimwezeshi mhitimu wa ngazi mojawapo kuendelea na elimu na mafunzo ya ngazi ya juu. Kila kozi ina muda wake, na maudhui yake hutofautiana kulingana na mahitaji ya kozi husika. Aidha, maudhui ya mitaala ya elimu ya ufundi na mafunzo hayatoshelezi katika kuleta muunganiko wa ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Upungufu huu ni kikwazo kwa mhitimu kujiendeleza na kushiriki katika kazi ambazo zinahitaji ujuzi wa juu zaidi.

Kuna umuhimu wa kuwa na mfumo wa sifa linganifu wa elimu ya ufundi na

61

Page 71: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

mafunzo (Technical and Vocational Education and Training Qualifications Framework) ili kuondoa vikwazo vya muunganiko na kujiendeleza katika elimu ya ufundi na mafunzo.

Madhumuni Kuwa na muunganiko wa maudhui katika mitaala ya elimu ya ufundi na ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.

Tamko

5.4.20 Serikali itaweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa mitaala kwa kozi zote za Elimu ya Ufundi na Mafunzo inarekebishwa na kuimarishwa na chombo husika ili kuleta muunganiko wa ngazi mbalimbali katika mfumo wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

5.4.21 Mitaala ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo itarekebishwa ili ikidhi mahitaji ya jamii na kuweka muunganiko kati ya ngazi moja na nyingine.

5.4.22 Serikali itahakikisha kuwa Elimu ya Ufundi na Mafunzo inayotolewa inakidhi mahitaji ya Sekta mbalimbali.

5.4.23 Mafunzo ya stadi za ujasiriamali yatakuwa ni sehemu ya programu zote za Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

SualaMatumizi ya teknolojia asili kwa maendeleo ya Jamii.

Maelezo Teknolojia za asili katika jamii ni hazina inayostahili kurithishwa na kuendelezwa. Teknolojia hii inatumia malighafi asili ambayo kama ikiendelezwa itachangia katika kuondoa umaskini katika jamii na kukuza uchumi wa taifa. Pamoja na umuhimu huo, mitaala ya Elimu ya Ufundi na

62

Page 72: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Mafunzo haijaingiza maudhui ya Teknolojia asili.

MadhumuniKuwa na Mitaala ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yenye maudhui ya Teknolojia za asili.

Tamko

5.4.24 Teknolojia asili zitabainishwa na kufungamanishwa katika mitaala ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

Elimu ya Juu

SualaUbora wa Mitaala ya Elimu ya Juu.

Maelezo Vyuo vikuu na baadhi ya vyuo vingine vya elimu ya juu vina mamlaka ya kuandaa na kuendeleza programu za mafunzo katika vyuo vyao. Aidha, mitaala ya baadhi ya vyuo huandaliwa na wizara inayosimamia chuo husika. Mitaala ya baadhi ya vyuo haina ulinganifu katika maudhui na muda wa mafunzo kwa programu zinazolingana na kufanana. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ndiyo inayohusika na utambuzi rasmi na uhakiki wa ubora wa programu zinazotolewa na vyuo vikuu. Aidha, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi linahusika na utambuzi rasmi wa vyuo vya elimu ya ufundi na program za mafunzo katika vyuo hivyo.

Kutokana na kukosekana kwa ulinganifu huo kuna uwezekano mkubwa wa

63

Page 73: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

programu kutolenga mahitaji ya jamii na kuathiri ubora wa elimu ya juu katika fani mbalimbali na soko la ajira. Kuna umuhimu wa kuimarisha uratibu na udhibiti wa ubora ndani ya asasi na kati ya asasi na asasi.

Madhumuni Kuwa na ulinganifu wa ubora wa mitaala katika programu mbalimbali za vyuo vya elimu ya juu.

Tamko

5.4.25 Serikali itaimarisha uratibu na udhibiti wa ubora wa mitaala ya asasi za elimu ya juu ili kuleta ulinganifu wa programu zitolewazo.

5.4.26 Serikali kwa kushirikiana na wadau itapanua na kuimarisha programu za mafunzo na tafiti za Sayansi na Teknolojia katika Vyuo vya Elimu ya Juu.

5.4.27 Serikali itaratibu uandaaji wa mitaala ya Elimu ya Juu inayokidhi mahitaji ya jamii na soko la ajira.

Elimu ya Watu Wazima

SualaMitaala ya Elimu ya Watu Wazima

MaelezoElimu ya watu wazima inatolewa chini ya Mfumo Rasmi na Nje ya Mfumo Rasmi kwa njia ya ana kwa ana na kwa masafa. Elimu hii inajumuisha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu na elimu ya kujiendeleza. Mitaala ya elimu na mafunzo hayo huandaliwa na kusimamiwa na wizara yenye dhamana ya elimu. Pamoja na kuwepo kwa mtaala na mkakati wa

64

Page 74: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

utekelezaji, bado elimu hiyo haijawafikia walengwa wengi.

MadhumuniKuwa na usimamizi na uratibu thabiti wa mitaala ya elimu ya msingi kwa watu wazima

Tamko

5.4.28 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaandaa mitaala ya elimu ya Watu Wazima na ya kujiendeleza inayokidhi mahitaji ya kundi hilo.

5.4.29 Serikali itaweka utaratibu wa kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Watu Wazima na ya elimu ya kujiendeleza.

Utafiti katika Elimu na Mafunzo

SualaUtafiti na Ubunifu katika Elimu na Mafunzo.Maelezo Ili kuimarisha taaluma na maendeleo katika elimu na mafunzo, hapana budi kuwa na utafiti. Misingi ya uandaaji na maamuzi ya kisera na miongozo hayana budi kuzingatia matokeo ya utafiti. Zipo tafiti nyingi zinazofanyika na taasisi mbalimbali zikiwepo za elimu, mashirika na wataalamu katika maeneo mbalimbali. Matokeo ya baadhi ya tafiti hizo ni ugunduzi, uvumbuzi na ubunifu ambao unastahili kutambuliwa, kumilikishwa na kuendelezwa kwa maendeleo ya taifa. Aidha, tafiti hizi hazina uratibu ambao ungewezesha

65

Page 75: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

kuondoa marudio yasiyo ya lazima na kuwezesha matokeo ya tafiti hizi kuwafikia walengwa kwa wakati na kutumika kwa maendeleo ya jamii.

Idadi ya Watumishi kwenye vitengo vingi vya utafiti vilivyopo hawatoshelezi na kiwango cha tafiti zinazofanywa hazitoshelezi mahitaji. Aidha, kuna rasilimaliwatu isiyotumika ipasavyo katika shule na vyuo ambayo inaweza kufanya utafiti unaofaa kwa maendeleo ya jamii za maeneo ambako taasisi hizi ziko. Taasisi za elimu ya juu hufanya tafiti kwa jitihada za kuongezea na kupanua upeo wa maarifa. Aidha, tafiti na tathmini zinazofanyika hazina mpangilio unaofaa na matokeo yake hayasambazwi kwa wadau mbalimbali kutokana na ukosefu wa uratibu. Kwa hiyo kuna umuhimu wa kurekebisha mazingira ya kufanya tafiti na usambazaji wa matokeo yake kwa walengwa ili kutumia vyema matokeo ya tafiti hizo kwa maendeleo ya nchi.MadhumuniKuwa na uratibu thabiti wa tafiti zinazofanyika katika sekta ya elimu na kuwezesha matokeo yake kutumika kwa maendeleo ya taifa.

Tamko

66

Page 76: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.4.30 Serikali itaweka utaratibu wa kuratibu tafiti zinazofanyika katika sekta ya elimu.

5.4.31 Serikali itaanzisha Kituo cha Taifa cha kukusanya, kutunza na kusambaza machapisho, na taarifa mbalimbali za tafiti za kielimu.

5.4.32 Serikali, kwa kushirikiana na wadau, itajenga na kuimarisha uwezo wa vitengo, shule, vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu kufanya tafiti zenye matokeo yatakayotoa ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yaliyopo katika jamii.

5.4.33 Utafiti wa Elimu utakuwa ni sehemu muhimu katika mitaala ya shule, vyuo na taasisi zote za elimu na Mafunzo.

5.4.34 Serikali itaimarisha uratibu wa kutambua, kumilikisha na kuendeleza ugunduzi, uvumbuzi na ubunifu katika elimu na mafunzo. (Intellectual Property Rights)

Sayansi na Teknolojia

SualaElimu ya Sayansi na Teknolojia katika shule na vyuo vya elimu na mafunzo.

MaelezoSayansi na teknolojia ni nyenzo muhimu katika kumwezesha binadamu kumudu mazingira yake na kumwezesha kuwa na maendeleo. Shule na vyuo vina majukumu muhimu ya kukuza elimu ya sayansi na teknolojia. Mitaala ya shule inaweka mkazo katika ufundishaji wa hisabati, sayansi yakiwemo masomo ya fizikia, kemia, biolojia, TEHAMA na stadi za msingi za teknolojia. Mitaala ya vyuo inaweka mkazo katika ufundishaji wa hisabati, TEHAMA na masomo ya ufundi wa fani mbalimbali. Katika vyuo vikuu, ufundishaji wa programu za sayansi na teknolojia unategemea aina na uwezo wa chuo husika.

67

Page 77: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Ufundishaji wa masomo katika shule na programu katika vyuo unakabiliwa na uhaba wa rasilimaliwatu, vifaa na miundombinu stahiki. Aidha, hakuna uwiano kati ya programu zinazotolewa na mahitaji halisi ya soko la ajira kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu wa kitaifa wa kubaini na kupanga maoteo ya rasilimaliwatu ikiwa ni pamoja na taaluma ya sayansi na teknolojia.

Madhumuni Kuwa na utaratibu endelevu wa utoaji wa elimu ya hisabati, sayansi na teknolojia shuleni na vyuoni.

Tamko

5.4.35 Serikali, kwa kushirikiana na wadau, itaimarisha ufundishaji wa hisabati, sayansi na teknolojia katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.4.36 Serikali itaweka utaratibu wa kuwa na mazingira rafiki ya kazi ya walimu, wakufunzi, na wahadhiri wa masomo ya hisabati, sayansi na teknolojia katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.

5.4.37 Serikali itahamasisha ushiriki wa wanafunzi wa jinsi zote katika, masomo ya Hisabati, Sayansi na Teknolojia na kuwaendeleza wenye vipaji na vipawa katika masomo hayo.

Sayansi Jamii

Suala

68

Page 78: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Mfumo wa utoaji wa elimu ya sayansi jamii unaokidhi mahitaji.

Maelezo Sayansi jamii humwezesha mtu kutambua wajibu na haki zake, kujitambua, kuelewa mabadiliko ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kiteknolojia. Sayansi jamii hufundishwa katika ngazi zote za elimu na mafunzo kwa njia ya masomo tofauti. Aidha, kuna upungufu wa ufundishaji wa sayansi jamii unaochagizwa na upungufu wa rasilimaliwatu, vitendea kazi na miundombinu stahiki. Kuna umuhimu wa kuimarisha utoaji wa elimu ya sayansi jamii ili ukidhi mahitaji ya wanafunzi na soko la ajira.

Madhumuni Kuwa na mfumo bora wa utoaji wa elimu ya sayansi jamii utakaokidhi mahitaji ya taaluma na utaalamu katika soko la ajira.

Tamko

5.4.38 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaimarisha utoaji wa elimu ya sayansi jamii katika mfumo wa elimu na mafunzo ili kukidhi mahitaji mbalimbali katika jamii.

5.4.39 Ufundishaji wa elimu ya sayansi jamii utakuwa ni wa lazima katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.4.40 Serikali itahakikisha kuwepo kwa uwiano stahiki katika masomo ya sayansi na sayansi jamii katika shule na vyuo kulingana na mahitaji ya taifa.

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

69

Page 79: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SualaTEHAMA katika utoaji wa elimu na mafunzo

MaelezoTEHAMA ni teknolojia ya habari na mawasiliano inayowezesha kuhifadhi, kubadilishana habari, kufundisha na kujifunzia, na kurushia matangazo kwa njia ya mtandao kwa kutumia mitambo ya teknolojia ya kisasa kama vile redio, televisheni, satelaiti, video, simu na kompyuta.

TEHAMA inawezesha upatikanaji wa maarifa na ujuzi kwa haraka na ufanisi ambao ni msingi madhubuti wa kupata utaalamu unaohitajika kwa maendeleo ya nchi.

Mahitaji ya TEHAMA katika ngazi zote za elimu yameongezeka kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na utandawazi. Hata hivyo, miundombinu na rasilimali zilizopo nchini na kwenye taasisi za elimu na mafunzo haikidhi mahitaji ya ongezeko la watumiaji na mabadiliko ya haraka ya teknolojia.

MadhumuniKuwa na miundombinu na rasilimali za kutosha na stahiki za TEHAMA katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

Tamko

70

Page 80: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.4.41 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaimarisha miundombinu na kuongeza rasilimali kwa matumizi ya TEHAMA katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.4.42 Serikali itahakikisha TEHAMA inaendelea kuwa sehemu ya mitaala ya elimu na mafunzo katika ngazi zote.

Michezo Shuleni na Vyuoni

SualaMichezo katika mitaala ya ngazi zote za elimu na mafunzo.

MaelezoMichezo ni muhimu katika kuimarisha afya ya mwili, akili na nidhamu. Aidha, michezo huburudisha; hujenga urafiki, uhusiano na ari ya ushindani; na pia husaidia katika kukuza vipaji. Mfumo wa elimu na mafunzo nchini hauna utaratibu madhubuti wa kushirikisha wanafunzi wa ngazi zote za elimu na mafunzo katika michezo. Aidha, miundombinu ya michezo katika shule na vyuo haikidhi mahitaji na hivyo kutoruhusu ushiriki wa kutosha kwa wanafunzi katika michezo.

MadhumuniKuwa na utaratibu madhubuti wa ushirikishaji, usimamizi na uendeshaji wa michezo katika ngazi zote za elimu na mafunzo. Tamko

71

Page 81: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.4.43 Serikali itahakikisha kuwa michezo inaendelea kuwa sehemu muhimu ya mitaala katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.4.44 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaweka utaratibu madhubuti wa ushirikishaji, usimamizi na uendeshaji wa michezo katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.4.45 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaweka utaratibu wa kuwa na shule maalumu za kukuza na kuendeleza vipaji katika michezo kwa ngazi zote za elimu na mafunzo

Vitabu vya Kiada na Ziada katika Shule na Vyuo

SualaUbora wa vitabu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule na vyuo vya ualimu.

Maelezo Miswada ya vitabu na vifaa vingine vya kielimu kwa ajili ya elimu ya msingi, sekondari na vyuo vya ualimu huandaliwa na waandishi mbalimbali kwa kutumia mihtasari ya masomo husika. Miswada hiyo huwasilishwa kwenye Kamati ya Ithibati ya Vifaa vya Kielimu ambayo hutoa ithibati kwa vitabu na vifaa vilivyofikia viwango vinavyohitajika. Utaratibu wa kutoa ithibati hauna ukomo wala madaraja ya ubora na hivyo kusababisha kuwepo kwa vitabu vingi vilivyopata ithibati kushindania soko. Shule huchagua vitabu vyake kwa kuzingatia kigezo cha kuwa na ithibati na hivyo kila shule kuwa na vitabu tofauti kwa masomo na madarasa husika. Hali hii inasababisha kutokuwa na ulinganifu wa ubora wa ufundishaji na ujifunzaji.

MadhumuniKuwa na ulinganifu wa ubora wa vitabu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule na vyuo vya ualimu.

72

Page 82: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Tamko

5.4.46 Serikali itaweka utaratibu wa kuwa na vitabu vya kiada vyenye ubora kwa kila somo na kila darasa kitaifa.

5.4.47 Serikali itaweka utaratibu wa kuwa na vitabu vya ziada na rejea kwa ajili ya kuhamasisha usomaji na ujifunzaji katika shule na vyuo.

5.4.48 Serikali itaweka utaratibu wa udhibiti wa ubora wa vitabu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia utakaosimamiwa na chombo kitakachokasimiwa madaraka hayo.

5.4.49 Serikali itahakikisha ununuzi wa vitabu, vifaa vya maabara na karakana, kemikali na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia unafanyika kitaifa; na kusambazwa katika shule na vyuo husika

Huduma za Maktaba

SualaHuduma za Maktaba.

MaelezoHuduma za maktaba ni moja ya nyenzo ya kufundishia na kujifunzia ambayo humwezesha mtu kupata maarifa, stadi na mwelekeo. Huduma hizi, hukuza tabia na mwenendo wa usomaji na kujifunza, kuimarisha ufundishaji na kuongeza maarifa. Huduma bora za maktaba zinatambulika kwa kuwepo kwa miundombinu stahiki, vitabu vya kutosha, watumishi stahiki; na fedha za kutosha kwa matumizi ya uendeshaji.

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ambayo ilianzishwa mwaka 1975

73

Page 83: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

inawajibika na utoaji wa huduma za maktaba kitaifa. Bodi hii inawajibika katika kupanga, kuanzisha na kutunza maktaba za umma; kuinua kiwango cha vitabu vya maktaba za shule na vyuo na kuendesha mafunzo ya ukutubi. Aidha, bodi hii ina wajibu wa kuhifadhi machapisho na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu huduma za maktaba.

Upanuzi wa elimu pamoja na kasi ya kukua kwa sayansi na teknolojia imefanikisha matumizi ya TEHAMA katika shughuli mbalimbali za uchapishaji. Hali hii imesababisha mfumuko mkubwa wa maarifa ambayo yako katika vitabu na machapisho mbalimbali. Kwa hiyo, matumizi ya maktaba yameongezeka na kuchukua sura mpya ya uendeshaji. Hata hivyo, bodi haijaweza kukidhi mahitaji ya umma kwa huduma zake kwenye ngazi za mkoa, wilaya, kata, kijiji, vyuo na shule na kusababisha udhaifu katika utoaji wa huduma za maktaba nchini.MadhumuniKuwa na huduma za kisasa za maktaba katika shule, vyuo na maeneo mengine katika jamii.

Tamko

5.4.50 Serikali itaweka utaratibu wa kuanzisha na kuendeleza maktaba za umma za kisasa zitakazokidhi mahitaji ya makundi yote ya jamii katika ngazi za Shule, Vyuo pamoja na Taifa, Mkoa, Wilaya, Kata, na Kijiji.

5.4.51 Serikali itaimarisha na kuongeza uwezo wa upatikanaji wa wakutubi kwa ajili ya ngazi zote za Elimu na Mafunzo.

5.5 Matumizi ya Lugha katika Elimu na Mafunzo

Suala Ufundishaji wa lugha.

74

Page 84: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

MaelezoLugha ni chombo cha mawasiliano na nyenzo muhimu ya kupata mbinu-tambuzi, maarifa, teknolojia, mitazamo na maadili. Hivi sasa, Kiingereza na Kiswahili ni lugha zinazotumika kwa kufundishia na kujifunzia katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Aidha lugha hizo, pamoja na lugha nyingine za kigeni, hufundishwa kama masomo. Pamoja na juhudi za kufundisha lugha hizo, bado kuna udhaifu wa kumudu lugha hizo katika ufundishaji na ujifunzaji. Sehemu kubwa ya udhaifu huo inatokana na mbinu duni za kufundishia, umahiri mdogo na matumizi madogo ya lugha hizo katika mazingira ya kawaida.

Lugha ya Kiswahili ambayo inatumiwa na wananchi wengi inawezesha kupata maarifa katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na sayansi na teknolojia. Aidha, lugha ya Kiingereza na lugha nyingine za kigeni zitawezesha watanzania kuwa na mawasiliano na mataifa mengine kuchangia katika kupata maarifa kwa kutumia lugha hizo. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuimarisha matumizi ya lugha za Kiswahili, Kiingereza na lugha nyingine za kigeni.MadhumuniKuimarisha matumizi ya lugha kwa ajili ya kuwasiliana, kufundishia na kujifunzia.

Tamko

5.5.1 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha ufundishaji wa lugha za Kiswahili, Kiingereza na lugha nyingine za kigeni katika mfumo mzima wa elimu na mafunzo.

Elimu ya Awali.Suala

75

Page 85: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Lugha ya Kufundishia.Maelezo Elimu ya awali inawaandaa watoto kuendelea kwa urahisi kwenye elimu ya msingi na kuimarisha kiwango cha maendeleo ya stadi za mawasiliano na ushirikiano miongoni mwao. Ili kuwezesha watoto hawa kujifunza dhana za msingi za elimu na mafunzo, ni muhimu kuwafundisha kwa kutumia lugha iliyokubalika rasmi kitaifa.

MadhumuniKuimarisha matumizi ya lugha za Kiswahili na Kiingereza ili kuwawezesha watoto kujifunza kwa ufanisi.

Tamko

5.5.2 Lugha ya kufundishia elimu ya awali itakuwa Kiswahili; na Lugha za Kiswahili na Kiingereza zitafundishwa kama somo.

Elimu ya Msingi.

Suala Lugha rasmi ya kufundishia Elimu ya Msingi

Maelezo Lugha rasmi ya kufundishia Elimu ya Msingi ni Kiswahili. Lugha ya Kiingereza hufundishwa kama somo la lazima. Matumizi ya lugha ya Kiingereza yanazidi kupanuka ulimwenguni kutokana na utandawazi, hali kadhalika matumizi ya Kiswahili nchini na katika mabara mengine yameongezeka. Kutokana na hali hii kumekuwa na mitazamo tofauti ya kijamii kuhusu lugha rasmi ya kufundishia Elimu ya Msingi. Mitazamo hii imeegemea katika lugha za Kiswahili na Kiingereza. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuimarisha matumizi ya lugha ya Kiswahili na kupanua matumizi ya lugha ya Kiingereza kama lugha

76

Page 86: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

za kufundishia elimu ya Msingi.

MadhumuniKuimarisha matumizi ya lugha za Kiswahili na Kiingereza ili kuwawezesha watoto kujifunza kwa ufanisi.

Tamko

5.5.3 Lugha za kufundishia Elimu ya Msingi zitakuwa Kiswahili na Kiingereza.

5.5.4 Lugha za Kiswahili na Kiingereza zitafundishwa kama somo.

Elimu ya Sekondari

SualaLugha rasmi ya kufundishia Elimu ya Sekondari.

MaelezoLugha ya kufundishia Elimu ya Sekondari ni Kiingereza. Tafiti mbalimbali zimeonesha kwamba binadamu huelewa vema dhana kama akijifunza kwa lugha anayoifahamu vizuri, na vyema zaidi kama ni lugha yake ya kwanza. Sehemu kubwa ya Dunia uzoefu unaonyesha kuwa jamii mbalimbali hutumia lugha zao kupatia maarifa na stadi mbalimbali na hufundishwa lugha za kigeni kwa ajili ya mawasiliano. Wanafunzi katika ngazi ya elimu ya sekondari hutumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza zaidi. Ili kuwezesha wanafunzi kuelewa dhana mbalimbali vizuri, lugha zinazotumika zaidi nchini zitatumika kupatia maarifa na stadi mbalimbali shuleni.

Madhumuni

77

Page 87: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Kuimarisha matumizi ya lugha za Kiswahili na Kiingereza ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa ufanisi.

Tamko

5.5.5 Lugha za kufundishia kwa ngazi ya Elimu ya Sekondari zitakuwa Kiswahili na Kiingereza.

5.5.6 Kiswahili na Kiingereza zitafundishwa kama lugha ya mawasiliano katika ngazi ya sekondari.

Elimu ya Ualimu

SualaLugha ya kufundishia elimu ya Ualimu.

MaelezoLugha ya kufundishia katika mafunzo ya Ualimu ngazi ya cheti ni Kiswahili na Kiingereza katika ngazi ya Stashahada na Shahada. Pamoja na kwamba lugha za kiingereza na kiswahili zinatumika kufundishia katika vyuo, bado hazijaweza kukuza stadi za mawasiliano kwa walimu wanaohitimu katika vyuo hivyo. Ili kuwezesha wanachuo kuelewa dhana mbalimbali vizuri, lugha zinazotumika zaidi nchini zitatumika kupatia maarifa na stadi mbalimbali vyuoni.

MadhumuniKuwa na mwalimu anayeweza kutumia lugha kwa ufasaha kufundisha dhana na maudhui yaliyoko katika mitaala.

Tamko

78

Page 88: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.5.7 Lugha za kufundishia elimu ya ualimu zitakuwa ni Kiswahili na Kiingereza.

5.5.8 Programu ya Stadi za Mawasiliano itakuwa ni ya lazima kwa elimu ya ualimu.

5.5.9 Serikali itaimarisha mafunzo ya lugha za Kiswahili na Kiingereza kwa walimu.

Elimu ya Ufundi na Mafunzo na Elimu ya Juu

SualaLugha ya kufundishia katika elimu ya ufundi na mafunzo na Elimu ya Juu.

MaelezoLugha ya kufundishia katika elimu ya ufundi na mafunzo na elimu ya juu ni Kiswahili na Kiingereza. Pamoja na kwamba lugha za kiingereza na kiswahili zinatumika kufundishia katika vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo na elimu ya juu, bado kuna umuhimu wa kuimarisha matumizi ya lugha hizo ili kuwezesha wanafunzi kuelewa dhana mbalimbali.

MadhumuniKuimarisha matumizi ya lugha za Kiswahili na Kiingereza ili kuwawezesha kupata wahitimu mahiri wa elimu ya ufundi na mafunzo na elimu ya juu.

Tamko

5.5.10 Lugha ya kufundishia elimu ya ufundi na mafunzo itaendelea kuwa Kiingereza na Kiswahili.

5.5.11 Lugha ya kufundishia elimu ya juu itakuwa Kiingereza na Kiswahili.

79

Page 89: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.6 Upimaji, Tathmini na Utoaji Vyeti

Upimaji katika elimu na mafunzo hutumia njia mbalimbali zikiwemo mitihani, mazoezi, majaribio na tasnifu/andiko. Matokeo ya upimaji huwezesha kutathmini utendaji wa mwanafunzi, mwalimu, shule au chuo katika utekelezaji wa mitaala. Aidha matokeo ya tathmini hutumika katika maamuzi ya kupanga, kuchagua na kutunuku vyeti.

Ili kuhakikisha uhalali katika upimaji na tathmini, kuna umuhimu wa kudhibiti mchakato mzima wa upimaji na tathmini ili kuleta ulinganifu katika utoaji elimu na mafunzo.

SualaUpimaji na tathmini ya Elimu na Mafunzo.

MaelezoKatika ngazi ya elimu ya msingi, mitihani rasmi miwili hutumika kwa wote mwishoni mwa Darasa la IV na Darasa la VII. Mtihani wa Darasa la IV huendeshwa kitaifa kwa usimamizi wa mkoa ili kubaini uwezo wa wanafunzi katika kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, na matokeo yake hutumiwa kufanyia uamuzi wa kutoa masomo rekebishi. Mtihani wa Darasa la VII ni mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na hutumiwa kwa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na elimu ya sekondari.

Katika ngazi ya elimu ya sekondari ngazi ya kawaida kunamtihani wa Kidato cha 2 ambao hutumiwa kupima utayari wa wanafunzi kuendelea na elimu ya sekondari. Aidha, hutoa fursa ya kuwabaini na kuwasaidia wanafunzi wenye uwezo mdogo ili waweze kukamilisha masomo ya sekondari. Mitihani ya Kidato cha 4 huhitimisha elimu ya Sekondari ya ngazi ya kawaida. Matokeo ya mtihani huu hutumiwa kwa uchaguzi wa wanafunzi kuendelea na elimu ya sekondari ngazi ya juu; elimu ya ufundi na mafunzo; na soko la ajira. Elimu

80

Page 90: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

ya sekondari ngazi ya juu ina mtihani wa Kidato cha 6 ambao huhitimisha elimu ya ngazi hii na hutumika kuchagua wanafunzi wa kujiunga na Elimu ya Juu, Elimu ya Ufundi na Mafunzo na soko la ajira.

Mitihani ya darasa la VII, kidato cha 4 na cha 6 huhitimisha utoaji wa elimu katika ngazi hizo. Aidha, ili upimaji wa mwisho uwe kipimo sahihi cha uwezo wa mwanafunzi na kipaji chake, hauna budi kujumuisha tathmini ya maendeleo ya kila siku na tathmini ya mwisho ya mwanafunzi.

Katika Elimu ya Ualimu kuna mitihani inayohitimisha mafunzo katika ngazi ya cheti na stashahada. Matokeo ya mtihani wa mwisho wa kuandika hujumuisha mazoezi na majaribio ya kila muhula kwa sehemu ya nadharia na mazoezi ya kufundisha (Block Teaching Practice – BTP) ili kuhitimisha mafunzo ya elimu ya ualimu ya cheti au stashahada.

Upimaji katika elimu ya ufundi na mafunzo unatumia njia mbalimbali ambazo hutofautiana kulingana na fani na aina ya kozi. Upimaji huo unafanywa na vyuo chini ya uratibu wa taasisi kadhaa zilizowekwa kisheria ambazo ni Baraza la Mitihani la Tanzania, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Upimaji na tathmini katika Vyuo vya elimu ya juu hufanywa na vyuo vyenyewe pamoja na taasisi zinazoratibu uendeshaji wa vyuo hivyo. Aidha, Vyuo Vikuu vina mamlaka ya upimaji, tathmini na utoaji tuzo baada ya programu zao kupewa ithibati na Tume ya Vyuo Vikuu. Hali hii inatoa mwanya wa kutokuwepo kwa ulinganifu katika viwango vya upimaji na tathmini kati ya chuo na chuo; na katika programu zinazofanana.

Kutokana na taasisi nyingi za Elimu ya Ufundi na Mafunzo kuhusika na upimaji na utoaji tuzo, kunahitajika uratibu thabiti wa mchakato huo ili kuleta ulinganifu wa tuzo. Aidha, kutokana na umuhimu wa upimaji na tathmini

81

Page 91: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

katika elimu na mafunzo, kuna umuhimu wa kuwa na utaratibu wa kitaifa wa kudhibiti upimaji na tathmini katika ngazi na programu mbalimbali za elimu na mafunzo.

MadhumuniKuwa na mfumo thabiti na uratibu wa upimaji na tathmni ya elimu na mafunzo

Tamko

82

Page 92: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.6.1 Serikali itaimarisha mfumo na utaratibu wa upimaji wa kitaifa wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.

5.6.2 Mamlaka yenye dhamana ya upimaji na utoaji vyeti itaratibu upimaji wa wanafunzi wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.

5.6.3 Matokeo ya upimaji wa wanafunzi wa Darasa la VI, Kidato cha 4 na Kidato cha 6 yatatumika kwa upangaji na uchaguzi wa wanafunzi kuendelea na elimu ya ngazi ya juu na mafunzo, kutolea cheti cha kuhitimu elimu ya ngazi husika na kwa ajira.

5.6.4 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha utaratibu wa upimaji na tathmini; na programu rekebishi kwa lengo la kubaini uwezo, utayari na kuwasaidia wanafunzi kuendelea na masomo katika ngazi mbalimbali.

5.6.5 Serikali itaimarisha utaratibu wa upimaji na tathmini ya EWW na ENMRA ili kubaini kiwango cha kisomo cha jamii.

5.6.6 Upimaji na tathmni ya kitaifa ya elimu ya ufundi na mafunzo utaratibiwa na mamlaka yenye dhamana ya upimaji na utoaji vyeti.

5.6.7 Vyuo vya elimu ya juu vitaendelea na utaratibu wa upimaji na tathmini kama itakavyoidhinishwa na mamlaka husika.

5.6.8 Serikali itaimarisha utaratibu wa upimaji na tathmini katika vyuo vya elimu ya juu ili kuleta ulinganifu katika tuzo zinazotolewa.

Utoaji Vyeti

Suala Udhibiti wa utoaji vyeti katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.

83

Page 93: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

MaelezoMhitimu wa elimu ya msingi hupewa cheti cha kukamilisha elimu ya ngazi hiyo bila kupata cheti cha tuzo kama ilivyo katika ngazi nyingine za elimu na mafunzo. Katika ngazi ya sekondari ya kawaida na ya Juu hutolewa vyeti vya aina mbili; cha kukamilisha elimu ya ngazi hiyo na kinachoonesha kiwango cha ufaulu wa mtahiniwa. Aidha, katika ngazi ya ualimu, hutolewa cheti cha kukamilisha elimu ya ngazi hiyo na cheti cha kuhitimu mitihani ya mwisho ambacho kinathibitisha ufaulu bila kuonesha kiwango cha ufaulu.

Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo hutoa vyeti vya aina tofauti kutegemeana na programu za ufundi husika. Vyeti vinavyotolewa katika vyuo hivyo hutofautiana kulingana na aina za fani na chuo kinachotoa tuzo hizo. Baadhi ya vyuo hutoa vyeti vyao na vyeti vingine hutolewa na mamlaka mbalimbali.

Vyuo vya Elimu ya Juu hutoa elimu na mafunzo ya aina tofauti kutegemeana na programu husika. Vyeti vinavyotolewa katika vyuo vya elimu ya Juu hutofautiana kulingana na aina za fani na chuo kinachotoa tuzo hizo. Kila chuo hutoa vyeti vyake. Hali hii inaweza kujenga mazingira ya vyeti vinavyotolewa kwa programu zinazofanana kukosa ulinganifu.

Sehemu kubwa ya elimu na mafunzo nje ya mfumo rasmi haitambuliwi kwa tuzo za vyeti. Kwa vile mafunzo haya yanalingana na mengine katika ngazi za mfumo rasmi wa elimu na mafunzo, ni vyema wahitimu nje ya mfumo rasmi wakatambuliwa na kupewa vyeti sawa na waliohitimu kwenye mfumo rasmi ili waweze kujiendeleza kwa urahisi katika mifumo ya elimu na mafunzo na kukubalika katika soko la ajira.

Katika hali ya ushindani uliopo ni muhimu kwa vyeti vinavyotolewa katika ngazi zote za elimu na mafunzo kuonesha viwango vya umahiri wa mhitimu.

84

Page 94: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Aidha, ili kuwa na vyeti stahili kwa sifa na ulinganifu katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo, ni muhimu kuwa na udhibiti thabiti wa vyeti vinavyotolewa.Madhumuni Kuwa na mfumo thabiti wa udhibiti wa utoaji vyeti katika ngazi zote za Elimu na Mafunzo.

Tamko

5.6.9 Utaratibu wa utoaji vyeti katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo utadhibitiwa na mamlaka yenye dhamana hiyo.

5.6.10 Msingi wa kupata cheti cha kuhitimu ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo utakuwa ni upimaji na tathmini ya kila siku na matokeo ya mwisho ya upimaji huo.

5.6.11 Utaratibu wa utoaji vyeti katika EWW na ENMRA utadhibitiwa na mamlaka iliyopewa dhamana hiyo.

5.6.12 Utoaji wa vyeti vya kuhitimu Elimu ya Ufundi na Mafunzo utadhibitiwa na mamlaka yenye dhamana ya upimaji na utoaji vyeti.

5.6.13 Vyeti vya kuhitimu Elimu ya Juu vitadhibitiwa na Mamlaka iliyopewa dhamana hiyo .

5.6.14 Mhitimu wa elimu na mafunzo nje ya mfumo rasmi atapata cheti cha ufaulu chenye kiwango kinacholingana na uhitimu kwenye ngazi hiyo ya mfumo rasmi.

Mitihani na Tuzo za Nje

Suala

85

Page 95: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Uratibu wa mitihani na udhibiti wa tuzo za nje.

Maelezo Baraza la Mitihani Tanzania linaratibu na kusimamia kufanyika kwa mitihani ya bodi mbalimbali za mitihani ya nje katika ngazi za taaluma na utaalamu. Aidha, baadhi ya shule na vyuo visivyo vya serikali hutumia mitihani ya nje kwa baadhi ya wanafunzi wake. Kutokana na kupanuka kwa teknolojia, baadhi ya watu wamekuwa wakifanya mitihani ya nje kupitia mtandao. Vile vile, kuna shule, vyuo na vituo ambavyo vinaendesha mitihani ya nje bila kutambuliwa rasmi. Hali hii inafanya udhibiti wa uendeshaji wa mitihani hiyo ya nje na wa viwango vya elimu na mafunzo wanavyofikia wanafunzi kuwa mgumu. Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kudhibiti mitihani ya nje inayofanyika hapa nchini ambayo haijarasimishwa na inayohusu watahiniwa wengi.

Madhumuni Kuwa na uratibu na udhibiti madhubuti wa Mitihani ya Nje.

Tamko

5.6.15 Serikali itaimarisha uratibu wa mitihani na udhibiti wa tuzo na vyeti vya nje katika ngazi zote za elimu na mafunzo kupitia mamlaka yenye dhamana hiyo.

5.7 Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu na Mafunzo

Usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo nchini ni jukumu la Wizara yenye dhamana ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Usimamizi na uendeshaji wa shule, vyuo na taasisi za elimu na mafunzo hufanywa kwa kushirikiana na wizara nyingine, mashirika na taasisi za Serikali na zisizo za Serikali. Vyuo vya ualimu vya Serikali vinasimamiwa na kuendeshwa na wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo. Aidha, usimamizi na uendeshaji wa shule za

86

Page 96: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

msingi na sekondari za Serikali unafanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Taasisi na mashirika yaliyopo chini ya wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo yana mamlaka kamili ya kuendesha shughuli zake bila uhusiano kisheria baina ya taasisi moja na nyingine. Hali kadhalika, mashirika na taasisi zisizo za serikali ambazo hutoa na kuendesha elimu na mafunzo husajiliwa na kutambuliwa rasmi na mamlaka za sekta tofauti. Kutokana na mahusiano yaliyopo na ukubwa wa sekta ya elimu na mafunzo, kuna umuhimu wa kuimarisha uratibu kwa kufungamanisha ngazi zote za elimu na sekta anuwai.

SualaUdhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali za Elimu na Mafunzo.

Maelezo

Wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo ina taasisi na mashirika yanayosimamia na kuratibu utoaji wa elimu na mafunzo. Kila taasisi na mashirika hayo yana bodi za utendaji ambazo hutoa maamuzi juu ya masuala ya utoaji na uendeshaji wa elimu na mafunzo katika maeneo ya mamlaka zao.

Taasisi hizo zina majukumu ya utambuzi rasmi wa vyuo, uandaaji wa mitaala, utoaji wa mitihani, tuzo na vyeti kwa pamoja katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Hali hii inaathiri ubora wa elimu na mafunzo yatolewayo. Aidha, zipo taasisi ambazo husimamia ubora wa elimu na mafunzo na wakati huo huo humiliki vyuo vinavyotoa elimu na mafunzo hayo. Matokeo yake ni mwingiliano wa majukumu unaoathiri uwajibikaji na ubora wa elimu na mafunzo yatolewayo. Hivyo, husababisha kutokutambulika kwa baadhi ya tuzo zitolewazo na kuleta ugumu wa

87

Page 97: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

kukubalika kwa wahitimu kuendelea na elimu na mafunzo katika ngazi zinazofuata.

MadhumuniKuwa na mfumo linganifu wa mitaala na utoaji tuzo katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.

Tamko

5.7.1 Serikali itaweka mfumo wa sifa linganifu wa Kitaifa wa utambuzi rasmi wa shule na vyuo, mitaala, upimaji na utoaji tuzo na vyeti kwa ngazi zote za Elimu na Mafunzo (National Education Qualifications Framework).

5.7.2 Serikali itaanzisha mamlaka ya kitaifa itakayosimamia utambuzi rasmi wa shule na vyuo; uandaaji wa mitaala; upimaji; utoaji tuzo na vyeti katika ngazi mbalimbali ili kuleta tija na ufanisi katika mfumo wa elimu na mafunzo.

5.7.3 Serikali itaongeza uwezo wa Bodi ya Huduma za Maktaba ya taifa wa kusimamia na kutoa huduma za kisasa za maktaba nchini.

SualaHuduma muhimu Shuleni na Vyuoni.

MaelezoShule na vyuo vingi nchini vina upungufu mkubwa wa huduma muhimu kama chakula cha mchana kwa shule za kutwa, maji safi na salama, afya na umeme. Lishe na afya bora kwa wanafunzi huongeza ushiriki katika elimu na mafunzo, hupunguza utoro na huongeza uwezo wa kujifunza. Pamoja na umuhimu huo, huduma hizi hazipatikani kwa kiwango kinachotosheleza. Kuna umuhimu wa kuwa na utaratibu madhubuti wa kutoa huduma muhimu shuleni na vyuoni ili kuinua ubora wa elimu na mafunzo.

88

Page 98: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

MadhumuniKuwa na huduma muhimu na endelevu shuleni na vyuoni.

Tamko

5.7.4 Serikali itahimiza wazazi, jamii, Serikali za Mitaa na wadau wengine kuhakikisha kuwa huduma ya chakula bora, mawasiliano, umeme, maji safi na salama, na afya zinapatikana katika shule na vyuo vya serikali na visivyo vya serikali.

Ushauri wa Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu na Mafunzo

SualaBaraza la Ushauri la Elimu na Mafunzo.

Maelezo Serikali inahitaji kushauriwa kwa upeo mpana katika masuala yanayohusu elimu na mafunzo. Ushauri huo unaweza kupatikana kwa kuwa na chombo ambacho kitajumuisha wadau wenye upeo na uzoefu wa elimu na mafunzo kutoka sekta za Serikali na zisizo za Serikali. Baraza la Ushauri la Elimu lililopo halina sekretarieti imara. Hali hii inasababisha baraza lishindwe kutoa ushauri ipasavyo.

MadhumuniKuwa na utaratibu endelevu wa kuishauri Wizara.

Tamko

89

Page 99: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.7.5 Serikali itaimarisha Baraza la Ushauri wa Elimu na Mafunzo kwa kuunda sekretariati imara ili liwe na uwezo wa kuibua hoja na kushauri Serikali ipasavyo kuhusu uendeshaji wa Elimu na Mafunzo nchini.

5.7.6 Serikali itaanzisha Baraza la Ushauri wa Elimu na Mafunzo katika Mkoa na Wilaya lenye uwezo wa kuibua hoja na kushauri ipasavyo.

Bodi za Asasi za Elimu

Suala Ushirikishaji wa jamii katika usimamizi na uendeshaji wa shule na vyuo.

Maelezo Uongozi na utawala wa asasi za elimu na mafunzo kwa sehemu kubwa umekuwa mikononi mwa asasi husika. Ushirikishaji wa jamii katika uongozi wa shule na vyuo ni mdogo na mara nyingi hutegemea utashi wa uongozi wa shule au chuo kuliko taratibu mahsusi za ushirikishaji. Ni muhimu kurekebisha mfumo huu kwa kuziimarisha Bodi/Kamati za asasi ili wakuu wa asasi wawajibike kwenye Bodi/Kamati zao. Aidha, wazazi ni wenza wakuu wa walimu katika kutoa elimu, mafunzo na malezi ya wanafunzi. Pale ambapo upo uhusiano mzuri kati ya mwalimu na mzazi maendeleo ya mwanafunzi yanakuwa mazuri. Kufanikiwa kwa asasi za namna hiyo ni suala linalowahusu wazazi na jamii kama linavyohusu walimu.

MadhumuniKuwa na ushirikishaji thabiti wa jamii katika usimamizi na uendeshaji wa shule na vyuo.

90

Page 100: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Tamko

5.7.7 Shule za msingi zitaendelea kuwa na Kamati za Shule; na shule za sekondari na vyuo vya ualimu na ufundi vitaendelea kuwa na Bodi zitakazosimamia uendeshaji wa shule na vyuo.

5.7.8 Kamati/Bodi za Shule na vyuo zitaanzisha vyama vya mahusiano mema kati ya wazazi/walezi na walimu (Parents/Guardians Teachers Associations) vitakavyounganisha wazazi na walimu.

Ardhi kwa Matumizi ya Kielimu

SualaHatimiliki za ardhi kwa Asasi za elimu na mafunzo.

MaelezoAsasi za elimu na mafunzo zinahitaji ardhi ya kutosha, mazingira ya amani, utulivu na usalama ili kuhakikisha utoaji wa elimu bora. Aidha, zinahitaji ardhi ya kutosha kwa mahitaji ya sasa na upanuzi kwa ajili ya maendeleo ya baadaye. Kumekuwepo na tabia ya uvamizi wa ardhi iliyotengwa na kugawiwa asasi za elimu na mafunzo za serikali na zisizo za serikali. Aidha, urasimu usiokuwa wa lazima huchelewesha upatikanaji wa hatimiliki kwa taasisi zisizo za serikali. Hali hii inarudisha nyuma juhudi za serikali za kushirikisha sekta binafsi katika utoaji wa Elimu na mafunzo. Ili kulinda ardhi inayomilikiwa na taasisi za elimu na mafunzo zisivamiwe, kuna umuhimu wa kuwa na hatimiliki kwa asasi zote za Elimu na Mafunzo.

Madhumuni Kuwa na asasi za elimu na mafunzo zenye hatimiliki za ardhi.

91

Page 101: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Tamko

5.7.9 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwa asasi za elimu na mafunzo zinakuwa na hatimiliki.

Uongozi na Utawala

SualaSifa stahiki za viongozi wa elimu na mafunzo.

Maelezo Uongozi na utawala bora ni muhimu kwa ufanisi wa mfumo wa elimu na mafunzo. Aidha, baadhi ya viongozi hawana sifa stahiki za kitaaluma na kitaalamu. Viongozi na watawala wa elimu na mafunzo kwenye ngazi za taifa, mkoa, wilaya na asasi hawana budi kuwa na uzoefu, sifa za juu kitaaluma na kitaalamu na ujuzi katika uongozi na utawala wa elimu na mafunzo.

MadhumuniKuwa na ufanisi katika utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo.

Tamko

92

Page 102: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.7.10 Viongozi wote wa elimu na mafunzo kwenye ngazi ya taifa, mkoa, wilaya na taasisi watawajibika katika uratibu wa mipango, utoaji, uendeshaji, utawala na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo katika mfumo rasmi na nje ya mfumo rasmi katika maeneo yaliyo chini ya mamlaka zao.

5.7.11 Viongozi katika asasi za ngazi za taifa, mkoa, wilaya, kata na katika asasi za elimu na mafunzo rasmi kuanzia shule za msingi watakuwa na sifa stahiki za kitaaluma, mafunzo ya kitaalamu katika elimu na uongozi pamoja na uzoefu unaotakiwa.

5.7.12 Nafasi za Afisa Elimu wa Mkoa, Wilaya na Kata zitapewa madaraka yote juu ya utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo rasmi, na yasiyo rasmi kwenye maeneo yaliyo chini ya mamlaka zao.

5.7.13 Nafasi za Walimu Wakuu; na Wakuu wa Shule na Vyuo zitatambuliwa katika muundo rasmi wa Wizara husika na zitakuwa na madaraka ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi hizo.

SualaUwajibikaji wa Viongozi wa elimu wa Halmashauri na mikoa.

MaelezoViongozi wa elimu ngazi ya Mkoa na Halmashauri huteuliwa na kupewa maelekezo ya kisera na wizara yenye dhamana ya kusimamia elimu. Kwa mujibu wa sheria ya elimu watendaji hawa wanawajibika kusimamia utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo katika maeneo yao. Kwa mujibu wa sheria ya Tawala za Mikoa, Afisa Elimu Mkoa ni mshauri wa elimu kwenye sekretarieti ya mkoa na anaripoti kwa Katibu Tawala wa Mkoa. Kwa mujibu wa sheria za Serikali za Mitaa, Afisa Elimu Wilaya ni mkuu wa idara ya elimu kwenye Halmashauri na huwajibika kwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Kwa

93

Page 103: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

hali hiyo utendaji wao katika kusimamia utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo huathirika kutokana na kuwajibika kwenye mamlaka zaidi ya moja kwa wakati mmoja.

MadhumuniKuwa na ufanisi katika utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo.

Tamko

5.7.14 Serikali itaweka utaratibu utakaowawezesha viongozi wa elimu ngazi ya mkoa na Halmashauri kutekeleza ipasavyo sera na sheria ya elimu na mafunzo kama inavyoelekezwa na wizara yenye dhamana ya elimu.

Suala Hadhi maalumu katika utumishi (superlative posts) kwa viongozi katika ngazi mbalimbali za Elimu na Mafunzo.Maelezo Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo husimamiwa katika ngazi ya kanda za elimu, mikoa, wilaya, kata, vyuo vya ualimu, shule za sekondari na msingi. Viongozi wa ngazi hizo hawapewi hadhi maalumu katika utumishi (superlative post). Hali hii inashusha hadhi katika usimamizi na inapunguza ari ya utendaji wao wa kazi. Kuna umuhimu wa kuinua hadhi ya nafasi zao ili kuimarisha usimamizi na utendaji wa kazi.

MadhumuniKuwa na wasimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo wenye hadhi maalumu katika utumishi.

Tamko

94

Page 104: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.7.15 Serikali itaweka utaratibu wa kutambua nafasi za usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi ya mkoa, wilaya, kata, vyuo na shule ili ziwe na hadhi maalumu katika utumishi.

SualaHuduma kwa walimu.

MaelezoWalimu hupewa mafunzo ya awali, mafunzo kazini na kupangiwa kazi na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Baada ya kuajiriwa walimu wa vyuo vya ualimu vya serikali hulipwa mishahara na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati wale wa shule za msingi na sekondari hulipwa mshahara na halmashauri. Walimu wote hupandishwa madaraja na Tume ya Utumishi wa Umma Idara ya Utumishi wa Walimu (TSD). Mamlaka hizi mbili zina mawasiliano hafifu kuhusu huduma wanazotoa kwa mwalimu. Hali hii inasababisha walimu kuchelewa kupata au kukosa stahili zao.

MadhumuniKuwa na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa walimu.

Tamko

95

Page 105: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.7.16 Serikali itaandaa utaratibu wa kumwezesha mwajiri wa walimu kuhusika na taratibu zote za kiutumishi za walimu.

5.7.17 Serikali itaanzisha chombo cha kitaalamu cha walimu kitakachohusika na usajili, kuendeleza walimu na kusimamia maadili ya taaluma ya ualimu.

5.7.18 Serikali itaweka utaratibu wa kuwatambua rasmi walimu wote wenye vyeti wa shule na vyuo vya serikali na visivyo vya serikali.

Suala Vituo vya Kuendeleza Walimu.

Maelezo Vituo vya kuendeleza walimu vinawezesha uimarishaji wa taaluma na utaalamu wa ualimu na ni sehemu ya kupatia maarifa na taaluma karibu na maeneo yao ya kazi. Vituo hivi huchochea ubunifu na uvumbuzi wa mbinu mpya za kufundishia na maandalizi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Aidha, vituo hivi hutoa nafasi ya kujiendeleza, kubadilishana mawazo na uzoefu wa kitaalamu baina ya walimu.

MadhumuniKuwa na vituo bora vya kutosha vya kuwaendeleza walimu.

Tamko

5.7.19 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaanzisha na kuimarisha vituo vya kuwaendeleza walimu katika ngazi ya kata kwa ajili ya matumizi ya walimu wa ngazi zote.

Suala

96

Page 106: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Menejimenti ya data za asasi za Elimu na Mafunzo.

Maelezo Ufanisi katika uongozi unategemea, kwa kiasi kikubwa, uwepo wa mfumo madhubuti wa uhifadhi wa data unganifu. Data ni muhimu katika kufanya maamuzi na kupanga mipango mbalimbali ya Elimu na Mafunzo. Aidha, katika kukasimu madaraka ya usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo, ni vema pawe na kumbukumbu muhimu za shughuli za elimu na mafunzo. Ni muhimu taarifa mbalimbali za Elimu na Mafunzo kuhifadhiwa vizuri ili ziweze kupatikana na kutumiwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Madhumuni Kuwa na mfumo madhubuti wa takwimu na menejimenti ya data unganifu za Elimu na Mafunzo.

Tamko

5.7.20 Wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo itaweka mfumo madhubuti wa takwimu na menejimenti ya data unganifu za asasi za elimu na mafunzo.

Suala Ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Maelezo Elimu ya Juu ni suala la muungano, wakati ngazi nyingine za elimu sio za muungano. Hata hivyo sekta za Elimu Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar zina uhusiano na ushirikiano katika maeneo ya mitaala na upimaji wa elimu

97

Page 107: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

ya ufundi na mafunzo katika ngazi ya ufundi sanifu na uhandisi/uteknolojia. Hali kadhalika, katika ngazi ya elimu ya sekondari na vyuo vya ualimu kuna uhusiano katika maeneo ya mitaala, upimaji na utoaji vyeti. Kwa kuzingatia uhusiano huu, upo umuhimu wa kuendelea kuimarisha uhusiano huo.

MadhumuniKuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kielimu kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Tamko

5.7.21 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaimarisha ushirikiano katika Elimu na Mafunzo.

Uwezo katika Utoaji wa Elimu na mafunzo

Uwezo wa utendaji katika elimu na mafunzo unajumuisha rasilimaliwatu, fedha, miundombinu na vitendea kazi. Baadhi ya viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali hawana sifa na ujuzi wa kutosha ili kutekeleza majukumu ya usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo.

Idadi ya watendaji katika ngazi zote za elimu na mafunzo haikidhi mahitaji na hakuna vitendea kazi vya kutosha. Aidha, kuna upungufu mkubwa wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, na miundombinu iliyopo ni chakavu na haitoshelezi. Hii ni pamoja na vyumba vya madarasa na vya mihadhara katika shule za msingi, sekondari, vyuo vya ualimu, vyuo vya ufundi, vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu, vifaa vya maabara na karakana. Hali hii inaathiri utoaji wa elimu bora.

Suala

98

Page 108: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Rasilimaliwatu.

MaelezoKutokana na kurasimisha Elimu ya Awali, kukua kwa mahitaji ya elimu katika jamii na ongezeko la idadi ya watu, mahitaji ya walimu wa Elimu ya Awali wenye sifa yameongezeka.

Ongezeko la idadi ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari limesababisha ongezeko kubwa la mahitaji ya Walimu. Aidha, sifa za sasa za kiwango cha cheti kwa walimu wa shule za msingi na stashahada kwa walimu wa shule za sekondari haziendani na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Hali kadhalika, kuna baadhi ya wakufunzi wa vyuo vya ualimu na vya ufundi ambao hawana sifa stahiki za kiwango kinachohitajika.

Katika elimu ya juu, kuna upungufu mkubwa wa Wahadhiri katika taaluma na fani mbalimbali. Hali hii inasababisha upungufu na udhaifu katika kuandaa nguvu kazi yenye utaalamu ili kukidhi soko la ajira. Aidha, watumishi hawapati mafunzo kazini ya kutosha ili kuwapa fursa ya kujifunza mbinu mpya katika kutekeleza majukumu yao na kuinua ubora wa utendaji kazi wao.

Kupanuka kwa sekta rasmi na isiyo rasmi kumeongeza shughuli nyingi za kiuchumi ambazo zinahitaji rasilimaliwatu iliyopata elimu na mafunzo bora ya ufundi na yenye stadi za ujasiriamali. Hata hivyo, katika sekta za uzalishaji na za utoaji huduma kuna upungufu mkubwa wa wataalamu bingwa.

MadhumuniKuwa na rasilimaliwatu yenye sifa na ujuzi kukidhi mahitaji.

Tamko

99

Page 109: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.7.22 Serikali itaweka utaratibu wa kupata rasilimaliwatu wenye sifa stahiki ili kukidhi mahitaji katika ngazi zote za Elimu na Mafunzo na soko la ajira.

5.7.23 Serikali itaweka utaratibu madhubuti wa mafunzo kabilishi na Mafunzo kazini kwa watumishi wa ngazi zote za Elimu na Mafunzo.

5.7.24 Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu, utaimarishwa na kuwa Chuo cha Menejimenti ya Utumishi wa Elimu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya menejimenti ya Elimu na mafunzo kwa ngazi zote za Elimu na Mafunzo.

5.7.25 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaweka mazingira ya kuwapata na kuwaendeleza wakutubi, wasaidizi wa maabara, mafundi sanifu wa maabara na wakufunzi wa Karakana.

5.7.26 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaweka utaratibu kwa wahitimu wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo kufanya kazi kwa mtindo wa kuambatishwa katika sekta binafsi na sekta za umma ili wajenge uzoefu.

Suala Upatikanaji wa Walimu katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

Maelezo Kuna upungufu wa walimu wenye sifa stahiki kwenye ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Hali hii inasababishwa na uwezo mdogo wa vyuo wa kuandaa walimu wanaokidhi mahitaji kitaalamu na kitaaluma. Aidha, baadhi ya walimu wanaacha kazi kutokana na mazingira ya ajira na kazi yasiyovutia. Upo umuhimu wa kuongeza nafasi na kuinua ubora wa mazingira ya ajira na kazi.

Madhumuni

100

Page 110: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Kuwa na walimu wanaotosheleza mahitaji.

Tamko

5.7.27 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaongeza nafasi za mafunzo ya Elimu ya Ualimu ili kukidhi mahitaji ya walimu kwa ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.7.28 Serikali itaendelea kushirikisha wadau katika kuinua ubora wa mazingira ya kazi, ajira na maslahi ya walimu.

Suala Miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.

Maelezo Uwepo wa miundombinu ya kutosha na stahiki ni muhimu katika kuinua ubora wa Elimu na Mafunzo katika ngazi zote. Miundombinu iliyopo katika shule, Vyuo na Taasisi nyingi za Elimu na Mafunzo ikiwemo majengo, mifumo ya maji na umeme imechakaa na haitoshelezi mahitaji. Pamoja na kuwepo kwa mipango ya maendeleo ya elimu na mafunzo, hakuna utaratibu endelevu wa kuhakikisha kuwa miundombinu inapatikana kulingana na ongezeko la watumiaji.

MadhumuniKuwa na miundombinu stahiki inayokidhi mahitaji ya wote katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

Tamko

101

Page 111: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.7.29 Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha uwepo wa miundombinu ya kutosha, stahiki na rafiki katika ngazi zote za Elimu na Mafunzo.

Suala Mitambo na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

MaelezoKuna upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na vya maabara na karakana katika ngazi zote za elimu na mafunzo. Aidha, vifaa vingi vilivyopo vimechakaa na hivyo kuathiri ufanisi wa utoaji wa elimu.

MadhumuniKuwa na mitambo na vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia vinavyokidhi mahitaji.

Tamko

102

Page 112: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.7.30 Serikali kwa kushirikiana na wadau, itaweka utaratibu wa kuwa na mitambo na vifaa stahiki vya kufundishia, kujifunzia na utafiti katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

5.7.31 Serikali itahamasisha utunzi, uchapishaji wa vitabu na utengenezaji wa vifaa vya kielimu kwa ajili ya wanafunzi na walimu wenye ulemavu.

5.7.32 Serikali itahamasisha watengenezaji wa ndani wa vifaa vya sayansi na karakana kwa ajili ya matumizi ya Elimu na Mafunzo.

5.7.33 Serikali itaandaa utaratibu wa kuwa na vitabu vya kutosha kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia kwa ngazi zote za Elimu na Mafunzo.

5.7.34 Vitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa madaraka hayo.

Ukaguzi wa Shule na Vyuo

Ukaguzi wa shule na vyuo ni uhakiki wa viwango vya ubora na mwenendo wa utoaji elimu na mafunzo kwa kuzingatia mitaala iliyopo na taratibu za uendeshaji.

Udhibiti wa ubora wa elimu itolewayo katika ngazi za awali, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu hufanywa na Idara ya ukaguzi wa shule iliyopo wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Vyuo vya ufundi stadi hukaguliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Aidha, taasisi za elimu ya juu hukaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi.

SualaUdhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo.

103

Page 113: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

MaelezoUdhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo katika shule na vyuo vya ualimu unafanywa na Wizara kwa kupitia idara ya Ukaguzi wa shule. Udhibiti huu hauna uthabiti na ufanisi unaostahili kutokana na idara hiyo kuwa sehemu ya Wizara inayokaguliwa utendaji wake. Aidha, Tume ya Vyuo Vikuu na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi vimepewa majukumu ya kuweka na kuhakiki viwango vya ubora wa elimu na mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya elimu ya ufundi, vyuo vikuu na vyuo vingine vya vya elimu ya juu. Utaratibu huu wa chombo kimoja kuweka viwango na kuhakiki ubora wa utekelezaji wake unapunguza ufanisi katika udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo.

MadhumuniKuwa na udhibiti thabiti wa ubora wa elimu na mafunzo yatolewayo nchini.

Tamko

5.7.35 Ukaguzi wa shule na vyuo katika ngazi zote za Elimu na Mafunzo utasimamiwa na mamlaka ya taifa ya sifa linganifu za elimu na mafunzo.

5.7.36 Serikali itahakikisha kuwa uteuzi wa wakaguzi wa shule na vyuo unazingatia sifa stahiki za kitaaluma, kitaalamu na uzoefu.

Ugharimiaji wa Elimu na Mafunzo Serikali inagharimia utoaji wa elimu na mafunzo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa ndani na nje. Kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya elimu na mafunzo jamii inawajibika kuchangia katika utoaji wa elimu kwa kuwa serikali peke yake haina uwezo wa kugharimia elimu na mafunzo. Ugharamiaji huo hufanyika kwa njia ya ruzuku inayotolewa na Serikali; misaada na mikopo inayotolewa na washirika wa maendeleo; ujenzi na

104

Page 114: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

uendeshaji wa shule unaofanywa na jamii na sekta binafsi na mashirika yasiyo ya serikali; karo, ada na michango mingine ya hali na mali inayotolewa na wazazi na wanafunzi.

SualaUgharimiaji wa elimu na mafunzo.MaelezoMoja ya majukumu ya serikali ni kutoa na kugharamia elimu kwa njia ya ruzuku ambayo hutokana na kodi. Mapato ya serikali hayatoshelezi kutoa huduma hiyo kwa ukamilifu. Kwa hiyo, jamii haina budi kutambua kwamba jukumu la kutoa elimu bora ni la wananchi wote na wanawajibika kutoa michango mbalimbali ili elimu na mafunzo yaweze kutolewa kwa ufanisi.

Madhumuni Kuwa na ugharamiaji fanisi wa elimu na mafunzo.

Tamko

105

Page 115: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

5.7.37 Serikali itaendelea kuiweka sekta ya elimu na mafunzo kuwa moja ya vipaumbele vikuu vya nchi.

5.7.38 Serikali itarekebisha muundo na mamlaka ya utoaji na urejeshaji wa mikopo kwa wanafunzi na kupanua wigo kwa kuhusisha vyombo mbalimbali vya fedha

5.7.39 Serikali itaendelea kuhamasisha sekta binafsi, jamii, wazazi na watumiaji wa elimu na mafunzo kuchangia gharama za elimu na mafunzo.

5.7.40 Serikali itaweka utaratibu wa kutumia gharama halisi za elimu na mafunzo kwa kila ngazi kama msingi wa kupanga ada na michango mbalimbali kwenye taasisi za elimu na mafunzo za serikali na zisizo za serikali.

5.7.41 Serikali itaweka utaratibu wa kuunganisha vyanzo vya rasilimali fedha za kugharimia elimu na mafunzo ili zitumike kulingana na vipaumbele vya elimu na mafunzo.

5.7.42 Mamlaka za Serikali za Mitaa zitatafuta vyanzo mbadala vya kugharamia elimu na mafunzo katika maeneo yao.

106

Page 116: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA YA 6

6.0 MASUALA MTAMBUKA

6.1 UtanguliziMasuala mtambuka katika elimu yanajumuisha jinsia, mazingira, VVU/UKIMWI, Ushauri na Unasihi, pamoja na Utawala Bora. Kwa kuwa masuala haya ni muhimu katika maendeleo ya taifa, hayana budi kuzingatiwa katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

6.2Jinsia katika Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu na Mafunzo

SualaUsawa wa kijinsia katika usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo.

MaelezoJinsia inahusu wajibu wa wanaume na wanawake katika jamii. Jinsia katika elimu na mafunzo inahusu usawa katika utoaji, usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo. Pamoja na juhudi ya Serikali kuhimiza usawa wa kijinsia katika uandikishaji wa wanafunzi, wasichana wanaomaliza elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu ni wachache kulinganisha na wavulana. Aidha, ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi mbalimbali za usimamizi na uongozi ni mdogo kutokana na mfumo dume katika jamii kuwa wanawake hawana uwezo sawa na wanaume. Kuna umuhimu wa kuweka usawa wa ushiriki katika usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo kwa ngazi zote.

MadhumuniKuwa na usawa wa kijinsia katika usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo.

Tamko

107

Page 117: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

6.2.1 Serikali itaweka utaratibu wa usimamizi na uongozi wa elimu na mafunzo unaozingatia sifa stahiki na uwiano wa kijinsia.

6.3 Elimu ya Mazingira na Afya ya Jamii

SualaUtunzaji wa Mazingira nchini.

MaelezoElimu ya mazingira na afya ya jamii ni elimu inayomwezesha raia kuelewa, kuthamini na kutunza mazingira. Aidha, elimu ya mazingira humwezesha raia kupata maarifa, stadi na mwelekeo utakaomsaidia kuwa mbunifu katika kutatua matatizo ya mazingira na kuongeza ubora wa afya ya jamii. Kuongezeka kwa idadi ya watu na shughuli mbalimbali za huduma ya kijamii na za uchumi zisizozingatia taratibu zinazofaa zimesababisha uharibifu wa mazingira nchini. Hii ni pamoja na ukataji ovyo wa miti, uchafuzi wa hewa, uharibifu wa vyanzo vya maji, utupaji ovyo wa taka maji, ngumu na za sumu; na matumizi mabaya ya ardhi yaliyokithiri katika maeneo mengi. Hali hii ikiendelea itahatarisha maisha ya binadamu na viumbe vilivyopo na kuathiri maendeleo ya nchi. Elimu itolewayo shuleni na vyuoni haina budi kuzingatia umuhimu wa kumwelimisha mwanafunzi ili kumjengea tabia na utamaduni stahiki kuhusu utunzaji wa mazingira na afya ya jamii.

MadhumuniKuwa na jamii yenye utamaduni wa kutunza mazingira na afya ya jamii.

Tamko

108

Page 118: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

6.3.1 Elimu ya mazingira na afya ya jamii itaendelea kuwa sehemu ya mitaala ya elimu na mafunzo katika ngazi zote.

6.3.2 Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kutoa elimu ya mazingira na afya ya jamii katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

6.4 Elimu ya VVU/UKIMWI na Athari za Matumizi ya Dawa za Kulevya

SualaMaambukizi ya VVU/UKIMWI na athari za matumizi ya dawa za kulevya.

MaelezoElimu kuhusu UKIMWI ina lengo la kutoa maarifa, stadi na mitazamo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI. Aidha, elimu hiyo hufundisha namna ya kuwahudumia na kuwafariji wanaoishi na walioathiriwa na VVU/UKIMWI. Juhudi za serikali za kudhibiti kuenea kwa VVU/UKIMWI hazijafanikiwa vya kutosha kutokana na watu wengi kutobadili tabia zao na hivyo kuendelea kutoa maambukizi mapya ya VVU. Kundi la rasilimaliwatu linaloathirika zaidi, wakiwemo wanafunzi, walimu na wafanyakazi wengine, ni la umri unaotegemewa kutoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya taifa. Aidha, mbali na wanaoishi na VVU/UKIMWI kuna waathiriwa wakiwemo yatima, wajane na watoa huduma na faraja. Hali hii inapunguza nguvu kazi yenye kuleta tija kwa taifa na kuathiri utoaji wa elimu na mafunzo. Pamoja na tatizo hili, matumizi ya dawa za kulevya yanachangia katika kueneza VVU/UKIMWI na kudumaza nguvukazi inayohitajika katika kukuza uchumi na huduma.

Elimu itolewayo shuleni na vyuoni haina budi kuzingatia umuhimu wa kumwelimisha na kumjengea mwanafunzi tabia na mwenendo stahiki kuhusu

109

Page 119: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

madhara ya dawa za kulevya na kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI, pamoja na kutoa huduma na faraja kwa walioathirika.

MadhumuniKupunguza kasi ya kuenea kwa maambukizi ya VVU/UKIMWI na kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya.

Tamko

6.4.1 Elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU na UKIMWI itaendelea kuwa sehemu ya mitaala ya elimu na mafunzo katika ngazi zote.

6.4.2 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU na UKIMWI katika ngazi zote za elimu na mafunzo ikiwa ni pamoja na huduma na faraja kwa wanaoishi na VVU/UKIMWI na waathiriwa.

6.4.3 Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutoa elimu ya kuepuka maambukizi ya maradhi mbalimbali ikiwemo Malaria na matumizi ya dawa za kulevya kwa wanafunzi katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

6.5 Huduma za Ushauri na Unasihi

SualaHuduma ya Ushauri na Unasihi shuleni na vyuoni.

MaelezoHuduma za ushauri na unasihi zinalenga katika kuwawezesha wanafunzi na

110

Page 120: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

jumuiya ya shule kwa ujumla kukabiliana na changamoto za maisha ili kujenga mwelekeo wa tabia na kuendeleza mila, desturi na maadili mema katika jamii. Kutokana na athari za utandawazi, kumekuwa na mwingiliano wa tamaduni na hivyo kusababisha kukosekana kwa maadili. Huduma za ushauri na unasihi zinahitajika kwa wanafunzi katika ngazi zote za elimu ili waweze kupata stadi za maisha za kujitambua na kufanya maamuzi sahihi katika kutekeleza wajibu wao kikamilifu na kujikinga na, au kuepuka matatizo ili kumudu masomo yao vizuri.

Serikali imeweka utaratibu wa kutoa huduma za ushauri na unasihi katika shule na vyuo. Hata hivyo utoaji wa huduma hiyo haukidhi mahitaji kutokana na upungufu wa wataalam.MadhumuniKuwa na huduma za kutosha za ushauri na unasihi katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

Tamko

6.5.1 Serikali itaimarisha huduma za ushauri na unasihi katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

6.5.2 Ushauri na unasihi vitaendelea kuwa sehemu muhimu ya mitaala ya Elimu ya Ualimu.

6.6 Utawala Bora

SualaUtawala Bora katika utoaji wa elimu na mafunzo.

MaelezoUtawala bora ni mfumo wa uongozi, usimamizi na uendeshaji unaozingatia utawala wa sheria, uadilifu, uwajibikaji, uwazi, ushirikishwaji na usawa ili

111

Page 121: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

kufikia malengo. Utawala Bora hauna budi kuzingatiwa katika uendeshaji na utoaji wa elimu na mafunzo katika ngazi zote. Viongozi na watumishi wengine katika elimu wanatarajiwa kuwa mfano wa kuigwa katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia utawala wa sheria, uwazi, usawa, uwajibikaji na ushirikishwaji ili kuinua ubora na ustawi wa maisha ya Mtanzania. Aidha, utawala bora ni muhimu katika kuwawezesha watendaji na wanafunzi kutumia vizuri rasilimali zilizopo ili kufikia malengo ya elimu na mafunzo. Kukosekana kwa maadili, kutowajibika ipasavyo kwa watendaji na wanafunzi husababisha kutofikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa. Kutozingatiwa kwa misingi ya utawala bora kumesababisha kukosekana kwa ushirikishwaji wa wanafunzi na wafanyakazi katika maamuzi ya kiutendaji shuleni na vyuoni na ukiukwaji wa haki za binadamu. Kuwepo kwa matukio ya vitendo vya rushwa na lugha zisizoridhisha kwa wateja kumepunguza ufanisi katika utendaji na kuongeza malalamiko kwa wadau wa elimu.

MadhumuniKuwa na utawala bora katika utoaji wa elimu na mafunzo

Tamko

6.6.1 Serikali itaimarisha utaratibu wa uwajibikaji, uwazi, usawa, utawala wa sheria, ushirikishaji na uadilifu katika utoaji wa elimu na mafunzo.

112

Page 122: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA YA 7

7.0 MUUNDO WA KITAASISI

7.1 UtanguliziSera ya Elimu na Mafunzo itatekelezwa katika ngazi za elimu ya awali, msingi, sekondari, ualimu, ufundi na elimu ya juu. Ili kufikia azma hiyo, Wizara yenye dhamana ya Elimu na Mafunzo itashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (OWM – TAMISEMI), Wizara nyingine, mashirika na Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, Washirika wa maendeleo wa ndani na nje, jamii na wadau wengine wa elimu na mafunzo. Aidha, Sera ya Elimu na mafunzo itatekelezwa kiutawala na kiutendaji katika ngazi za; Taifa, Mkoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Kata, Shule na Vyuo.

7.2 Ngazi ya Taifa Katika kutekeleza sera ya elimu na mafunzo, wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo itakuwa na muundo wa kitaasisi utakaojumuisha idara za elimu ya awali, msingi, sekondari, elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi, ualimu, ufundi na elimu ya juu. Aidha, wizara itashirikisha wizara yenye dhamana ya tawala za mikoa na serikali za mitaa pamoja na wizara na taasisi nyingine zinazojihusisha na utoaji wa elimu na mafunzo. Ushirikiano huo utahusu uchambuzi wa sera; kuweka viwango na kuandaa sheria, kanuni, miongozo na taratibu za utekelezaji wa sera; kuandaa mipango mikuu ya elimu na mafunzo, kufuatilia, kupima na kutathmini utekelezaji wake.

7.3 Ngazi ya MkoaJukumu la usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi ya Mkoa litakuwa la Afisaelimu Mkoa (Regional Education Officer - REO). Afisaelimu Mkoa atapokea na kusimamia utekelezaji wa kanuni, miongozo, na taratibu mbalimbali za utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo kutoka kwa Kamishna wa Elimu. Afisaelimu Mkoa atasimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika eneo lake la usimamizi.

113

Page 123: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

7.4 Ngazi ya Mamlaka za Serikali za MitaaMamlaka za Serikali za Mitaa zitahusika katika usimamizi na uendeshaji wa shule za msingi na sekondari na kutoa taarifa ya utekelezaji kwa ngazi za mkoa na Taifa. Katika ngazi hii kutakuwa na Afisaelimu anayeshughulikia Shule za Msingi na Afisaelimu anayeshughulikia Shule za Sekondari. Aidha, Maafisaelimu wa Halmashauri watasimamia na kuratibu utekelezaji wa Elimu Nje ya Mfumo Rasmi katika maeneo wanayosimamia. Wote watasimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu za usimamizi na uendeshaji wa shule za Serikali na zisizo za Serikali. Katika kutekeleza jukumu hilo, Afisaelimu atatakiwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri, Maafisaelimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari na Shule za Msingi za Serikali na zisizo za Serikali, Mashirika na Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali katika ngazi ya Halmashauri.

7.5 Ngazi ya KataKatika ngazi ya Kata, utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo utasimamiwa na Afisaelimu Kata ambaye atakuwa mratibu wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa Shule za Serikali na zisizo za Serikali katika ngazi ya shule za awali na msingi, elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi. Afisaelimu Kata atawajibika kwa Afisaelimu wa Halmashauri.

7.6 Ngazi ya Shule na VyuoWakuu wa shule za msingi na sekondari watasimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi za shule na watawajibika kutoa taarifa za utekelezaji kwa Afisaelimu Kata. Wakuu wa vyuo vya ualimu, elimu ya ufundi na mafunzo na vyuo vya elimu ya juu watasimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika vyuo vyao na kutoa taarifa za utekelezaji kwa mamlaka zilizo juu yao.

114

Page 124: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA YA 8

8.0 MUUNDO WA KISHERIA

8.1 Utangulizi Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unahitaji muundo wa kisheria utakaowawezesha wahusika kutekeleza majukumu yao. Hivyo, sheria mbalimbali zinazohusu elimu na mafunzo nchini zitapitiwa upya na kufanyiwa marekebisho. Mapitio ya sheria hizo yatazingatia muundo wa taasisi mpya zitakazoanzishwa katika sera hii na makubaliano yaliyopo kwenye mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa juu ya haki ya kupata elimu.

Sekta za Serikali na zisizo za serikali zinazojishughulisha na utoaji wa elimu na mafunzo zitatakiwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayotolewa katika kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo.

8.2 Vyombo vya KisheriaKutakuwepo na vyombo vya kisheria katika ngazi zote za usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo.

8.3 Baraza la Taifa la Ushauri wa Elimu na Mafunzo Kutakuwa na Baraza la Kitaalamu la kumshauri Waziri kuhusu Elimu na Mafunzo. Mwenyekiti wa Baraza hilo atateuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Elimu na Mafunzo. Vikao vya Baraza vitaandaliwa na Sekretarieti ya Baraza.

8.4 Chombo cha Kudhibiti Ubora wa UalimuKutakuwa na chombo cha kudhibiti maadili, taaluma na utaalamu wa walimu. Chombo hicho kitasajili na kufuta usajili wa walimu wa ngazi zote, wa serikali na wasio wa serikali. Mkuu wa chombo hicho atateuliwa na kuwajibika kwa Katibu Mkuu wa wizara yenye dhamana ya elimu.

115

Page 125: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

8.5 Mamlaka ya Taifa ya Sifa Linganifu za Elimu na Mafunzo (National Education Qualifications Authority)

Kutakuwa na Mamlaka ya Taifa ya Sifa Linganifu za Elimu na Mafunzo ambayo itasimamia na kuendesha shughuli za: usajili na ukaguzi wa shule na Vyuo vya Ualimu; utambuzi rasmi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo; Mitaala; Upimaji na utoaji wa tuzo. Mkuu wa Mamlaka atateuliwa na Rais na atawajibika kwa Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo.

8.6 Bodi ya Huduma za Maktaba (Tanzania Library Services Board - TLSB)

Kutakuwa na bodi ya huduma za maktaba itakayosimamia na kuendesha huduma za maktaba katika ngazi za taifa, mkoa, wilaya, kata na kijiji. Aidha, bodi itatoa ushauri wa kitaalamu kwa maktaba za taasisi za serikali na zisizo za serikali; itaendesha mafunzo ya ukutubi kama watakavyotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Elimu. Mkuu wa bodi hii atateuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya Elimu na Mafunzo na atawajibika kwa katibu mkuu wa wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo.

8.7 Baraza la Chuo KikuuKutakuwa na Baraza la Chuo katika kila Chuo Kikuu ambalo litahusika na utawala na udhibiti wa chuo. Mwenyekiti wa baraza hili atateuliwa na Rais.

8.8 SenetiKutakuwa na Seneti katika kila Chuo Kikuu itakayoshughulikia masuala ya taaluma na itawajibika kwa Baraza la Chuo. Mwenyekiti wa seneti atakuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo husika kutokana na wadhifa wake.

116

Page 126: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

8.9 Bodi za Vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo

Kutakuwa na bodi za vyuo katika kila Chuo cha Elimu ya Juu na Chuo cha Elimu ya Ufundi na Mafunzo. Bodi hizo zitasimamia mipango na maendeleo ya vyuo, matumizi ya fedha, nidhamu ya wanafunzi na maendeleo ya taaluma. Wenyeviti wa bodi hizo watateuliwa na Rais.

8.10 Bodi ya Rufaa ya MkoaKutakuwa na Bodi ya rufaa katika kila Mkoa ambayo itasikiliza rufaa ya mwanafunzi yeyote ambaye hakuridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na Bodi ya rufaa ya Halmashauri.

8.11 Bodi ya Rufaa ya HalmashauriKutakuwa na Bodi ya Rufaa katika kila Halmashauri ambayo itasikiliza rufaa ya mwanafunzi yeyote ambaye hataridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na Kamati au Bodi ya Shule.

8.12 Bodi ya Shule na Chuo cha UalimuKutakuwa na Bodi ya Shule katika kila Shule ya Sekondari na Chuo cha Ualimu ambayo itasimamia mipango ya maendeleo, matumizi ya fedha, nidhamu ya wanafunzi na maendeleo ya taaluma.

8.13 Kamati ya ShuleKutakuwa na kamati ya Shule katika kila Shule ya Msingi ambayo itasimamia Mipango ya maendeleo, matumizi ya fedha, nidhamu ya wanafunzi na maendeleo ya taaluma.

117

Page 127: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

SURA YA 9

9.0 MWISHOSera hii ya Elimu na Mafunzo ni sera shirikishi katika maandalizi na utekelezaji wake. Wadau wameainisha matatizo, upungufu na changamoto zilizoikabili jamii katika utekelezaji wa sera katika Karne ya 21 na hali ya mabadiliko ya haraka ya Sayansi na Teknolojia.

Wadau wamebaini masuala mbalimbali ambayo ama hayakuwepo kabisa, au hayakutekelezwa kabisa au hayakupewa uzito stahili katika Sera za Elimu na Mafunzo. Kwa hiyo, kuna haja ya kuondoa kasoro hizo katika utekelezaji wa sera hii. Tathmini ya Sera za Elimu na Mafunzo ilibaini udhaifu katika mfumo na muundo wa kisheria na kitaasisi; uwezo wa rasilimaliwatu; miundombinu na ugharimiaji wa elimu na mafunzo katika utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo. Hivyo, kuna umuhimu wa kufanya mapitio ya baadhi ya sheria na miundo ya kitaasisi ili kukuza na kuendeleza mawasiliano ndani ya wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo, baina ya wizara na taasisi zake na kati ya wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo na wizara nyingine. Serikali itajenga uwezo wa rasilimaliwatu; kuimarisha muundo wa kitaasisi na kisheria na uwezo wa kugharimia elimu na mafunzo ili kuwezesha utekelezaji fanisi wa Sera yaw Elimu na Mafunzo.

Mfumo wa elimu na mafunzo unapaswa kuwa shirikishi na unaojali wanafunzi, watendaji na wadau wengine katika ngazi na sehemu mbalimbali za elimu na mafunzo. Aidha, mfumo wa elimu na mafunzo hauna budi kuwa na muunganiko stahiki utakaoleta ufanisi katika utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo. Mfumo huo unatakiwa kumwezesha mwanafunzi kupata elimu bila vikwazo na watendaji kutekeleza wajibu wao na kupewa haki zao stahiki kwa wakati. Hii italeta ufanisi katika utoaji wa elimu na mafunzo.

Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo utahitaji maandalizi thabiti.

118

Page 128: MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA SERA YA ELIMU … · Web viewVitabu vya kiada, ziada na rejea kwa ajili ya ngazi za elimu ya msingi na sekondari vitapewa ithibati na mamlaka iliyokasimiwa

Mikakati na mipango mbalimbali itaandaliwa kwa kuzingatia matakwa ya Sera. Watekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi zote watapewa miongozo ili kupata uelewa na ufafanuzi wa kutosha wa madhumuni, maudhui na matarajio ya Sera. Utaratibu huu utawezesha utekelezaji fanisi wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi zote.

Utekelezaji fanisi wa Sera ya Elimu na Mafunzo utahitaji mfumo thabiti wa ufuatiliaji na tathmini. Ufuatiliaji na tathmini utafanywa na kila mdau na kila ngazi kwa kuzingatia viashiria stahiki vya Elimu na Mafunzo katika ngazi husika. Aidha, kutakuwa na ratiba ya ufuatiliaji na tathmini ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu na taarifa yake itatumika katika kupima ufanisi na kufanya maamuzi rekebishi. Aidha, mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ni nyenzo muhimu itakayopima nchi iko wapi, imetoka wapi na inakwenda wapi katika utoaji wa elimu na mafunzo.

119