uamsho-press-conference-25-05-2013.pdf

Upload: mzalendonet

Post on 03-Apr-2018

223 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 7/28/2019 uamsho-press-conference-25-05-2013.pdf

    1/6

    1

    JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU

    (JUMIKI)

    THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATIONP. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145-

    FAX +255-024-2250022 E-M ail:jumi ki@hotmai l.comMKUNAZINI ZANZIBAR

    25 Mei, 2013

    Bismillahir Rahmanir Rahiim

    TAARIFA JUU YA HALI HALISI NA MATUKIO YA KESI

    INAYOWAKABILI VIONGOZI WA UMOJA WA JUMUIYA NA TAASISI

    ZA KIISLAM, ZANZIBAR. 25 MEI, 2013

    Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam - JUMIKI, ni Jumuiya iliyosajiliwa kihali

    kufanya shughuli zake hapa Zanzibar mwaka 2001. Kwa kipindi chote hicho hadi kufikia

    tarehe 21/10/2012 JUMIKI ilikuwa ikiendelea kufanya shughuli zake kwa utulivu na

    amani na kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi na taratibu zilizowekwa.

    Wakati Jumuiya ikiendelea na kazi zake za kuhubiri, kutetea na kusimamia haki za

    Waislam na kuelimisha jamii juu ya maswala mbali mbali ya kidini na kijamii, mnamo

    mwezi wa Ogasti 2012 ilitokea kadhia ya kukamatwa Sheikh Mussa Juma wa Msikiti wa

    Biziredi. Baada ya hapo Waislam walijaribu kufatilia sababu za kukamatwa kwake na

    kushindikiza kuachiwa huru kwa kuwa hakukuwa na sababu ya kuwekwa ndani. Lakini

    kilichofuata ni mfululizo wa mabomu ya machozi na pilipili kuwatawanya hali

    iliyozidisha mtafaruku katika mji wa Zanzibar.

    Tarehe 19 Oktoba 2012 Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara na baadaye kuachiwa

    tarehe 22/10/2012. Tarehe 23 Oktoba 2012 Sheikh Farid alitakiwa afike Kituo cha Polisi,

    Madema kwa mahojiano kuhusu kutekwa nyara kwake. Masheikh wengine - Sheikh

    Msellem, Sheikh Azzan, Sheikh Mussa Juma na Sheikh Hassan walikwenda

    mailto:[email protected]:[email protected]:[email protected]:[email protected]
  • 7/28/2019 uamsho-press-conference-25-05-2013.pdf

    2/6

    2

    kumshindikiza. Bahati mbaya Polisi wakawakamata wote na kuwaweka ndani na

    kuwafungulia mashtaka mbali mbali ya uchochezi na uvunjifu wa amani na uharibifu wa

    mali na kupandishwa mahakamani tarehe 25 Oktoba 2012; siku ambayo masheikh wote

    walinyolewa ndevu zao, tukio lililowashangaza wengi kwani ule msingi wa Katiba

    kwamba hakuna mwenye hatia mpaka apatikane na hatia na Mahkama iliyo huru

    ulishavujwa tokea siku ya mwanzo kabisa.

    Baada ya hapo mashtaka kadhaa yakafunguliwa katika mahkama mbali mbali ikiwemo

    Kwerekwe (mahkama mbili za Wilaya), Mfenesini na Vuga (Mahkama Kuu). Dhamana

    ziliwekewa masharti magumu mwanzoni lakini baadae masharti yakalainishwa na

    washtakiwa kupewa dhamana katika kesi zote isipokuwa ile ya Mahkama Kuu. Kwa

    upande mwengine, kesi moja ya Mahkama ya Wilaya Kwerekwe ikafutwa na ile ya

    Mfenesini pia ikafutwa na Mkurugenzi wa Mashtaka.

    Kesi zote zinazowakibili Masheikh wa Uamsho ni kesi ambazo dhamana ni haki ya

    washtakiwa kwani makosa wanayoshtakiwa si makosa ambayo hayana dhamana. Aidha,

    kwa mujibu wa Sheria, kesi hizo zinapaswa kuanza ndani ya miezi minne, vyenginevyo

    inabidi washtakiwa wapewe dhamana. Kinyume na misingi yote ya sheria na haki,

    washtakiwa wote kumi wameshakaa ndani kwa zaidi ya miezi saba sasa kinyume na

    sheria na taratibu zote za kuendesha mashtaka ya jinai. Jambo hili la kuendelea kuwekwa

    mahabusu na kunyimwa dhamana kwa Masheikh ni dhulma, ukandamizaji na uvunjwaji

    wa makusudi wa haki za binaadamu. Jee hii ndio demokrasia na utawala bora?

    Lengo la Jumuiya sio kuingilia kazi za mahkama, bali tunahaki ya kikatiba ya kupinga

    uvunjifu wowote wa Katiba ya Zanzibar ya 1984. Kwa kawaida inapotokea uonevu kama

    huu tumekuwa tukishuhudia Jumuiya za Kitaifa na za Kimataifa, Taasisi za kutetea Haki

    za Binaadamu, Vyombo vya habari duniani, Asasi za Kijamii, Vyama vya wanasheria na

    wengineo wakipaza sauti zao kulaaani, kushtumu na hata kukemea waziwazi dhulma

    hizo; lakini kwa masikitiko makubwa hali imekuwa ni tofauti kwa Viongozi

    waliokumbwa na kadhia hii. Jee taasisi hizo ziko wapi? Au kwa sababu wahusika ni

    Viongozi wa Kiislam?

  • 7/28/2019 uamsho-press-conference-25-05-2013.pdf

    3/6

    3

    Ikumbukwe kama hawa ni viongozi wa juu wa Jamii kubwa ya Kiislam nchini, hivyo kila

    mtu linamgusa na kumuuma jambo ambalo likiendelezwa linaweza kusababisha uvunjifu

    wa amani usiotarajiwa. Kwa hali hii Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam

    (JUMIKI) imewaita Wanahabari, Mabalozi wa chi za nje, na Wadau mbali mbali

    kuwaeleza jinsi ya dhulma, ukandamizaji, na uonevu unavyoendelea dhidi ya Viongozi

    wetu kama ifuatavyo.

    Kuwatupia shutma kali na malamiko Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibarna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuvunja sheria za nchi

    walizozitunga na kuzilia viapo na kuzipitisha wenyewe na kudai kuwa hakuna

    mtu alie juu ya sheria.

    Jumuiya ya Kimataifa; wakiwemo:-Mabalozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya, Marekani, na Magharibi kwa ujumla kwa

    kukaa kimya kinyume na kawaida yao ya kutetea haki za binaadamu.

    Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali ndani na nje ya nchi Kwakutoripoti au kuripoti habari kwa kuegemea upande mmoja wa Serikali huku

    ikiihusisha Jumuiya na ufanyaji wa fujo, na pili kutoa habari kwa mitazamo yaowenyewe mfano; Kulihusisha tukio la Maandamano ya Morogoro na matukio ya

    Zanzibar.

    Rais wa Zanzibar kuendelea kuingilia uhuru wa Mahkama kwa kutoa misimamoyake mikali dhidi ya Masheikh wa Uamsho waliopo mahabusu.

    Kuvunjwa kwa katiba ya nchi mfano; kuingiliwa uhuru wa habari na maoni kwajeshi la polisi kukama CD za mawaidha ya kiislam na kuzuia redio kutangaza

    matangazo ya Jumuiya na Kamisheni ya Habari ya Zanzibar na Waziri wa

    Mambo ya ndani Mhe: Emanuel Nchimbi kuzuia kutoa taarifa za JUMIKI katika

    vyombo vya habari. Mfano: Redio Nour na Adhana FM.

  • 7/28/2019 uamsho-press-conference-25-05-2013.pdf

    4/6

    4

    Shutma kwa vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, naVikosi vya SMZ, kwa kupachuliwa kwa nguvu bendera za Jumuiya katika

    sehemu mbali mbali nchini kwa lengo la kuudhalilisha UISLAM, kupigwa na

    hata kuuliwa baadhi ya watu kwa kukataa kupachua bendera hizo.

    Matumizi ya nguvu kubwa, kuweka hali ya hatari, taharuki na kuzuia hata jamaaza washtakiwa kukaribia mahkamani ambapo hata kesi ya uhaini ndugu na jamaa

    waliruhusiwa kuhudhuria na kusikiliza kesi za ndugu na jamaa zao.

    Unyanyasaji wa watuhumiwa na uingiliaji wa uhuru wa kuabudu kwa mujibu wakatiba; Mfano; kuwanyoa ndevu kwa lazima, kuwazuia kusoma quraan, kupata

    habari, kuswekwa na kutengwa katika chumba cha kila mtu peke yake (katika

    siku za mwanzo za mahabusu).

    Kuwatenga na mahabusu wengine hata katika ibada kinyume na utaratibu washeria na haki za binaadamu.

    Mwisho, Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu inatoa TAMKORASMI kuhusiana na kadhia yote tangu ilipoanzia na hadi leo hii kama

    ifuatavyo;

    1. Jumuisha ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI),inakanusha vikali propaganda zote zinazoenezwa na vyombo vya habari,

    wanasiasa na watu mbali mbali kuihusisha Jumuiya na vurugu na vitendo

    vyovyote vile vya uvunjifu wa amani kama vile uchomaji wa makanisa,

    maskani na upotevu wa maisha ya watu. Fujo sio sera ya Jumuiya wala

    haihusiki nazo.

    2. Kwa vile Msingi mkuu wa katiba zote za nchi zinazoendeshwa kwa misingiya kidemokrasia ikiwemo Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ni kuheshimu na

  • 7/28/2019 uamsho-press-conference-25-05-2013.pdf

    5/6

    5

    kulinda haki za binaadamu ikiwemo uhuru wa kuabudu na kujikusanya na

    kujieleza, kwahiyo, JUMIKI inalaani vikali wale wote wanaotoa kauli za

    vitisho na matamko ya uvunjifu wa katiba na kuipeleka nchi katika utawala

    wa kidikteta.

    3. JUMIKI itaendelea na shughuli zake za kuelimisha, kutetea na kusimamiahaki na wajibu wa kila raia kama kawaida yake, ilimradi haivunji sheria wala

    taratibu za nchi. Itaendelea kutetea, kudai na kuelimisha umma wa

    Wazanzibari juu ya haki yao ya kuidai Zanzibar huru yenye mamlaka yake

    kamili kitaifa na kimataifa.

    4. JUMIKI inashangazwa na kauli za nchi za magharibi kwa kuipongeza Serikaliya Umoja wa Kitaifa; serikali ambayo inavunja na inakandamiza wananchi

    wake wenyewe kwa kudai haki yao ya kujitawala.

    5. JUMIKI itaendelea kusimamia agenda yake ya msingi ya kudai Zanzibar hurukinyume na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) na

    vyama vya kisiasa za kututoa katika lengo kwa kuanzisha agenda za pembeni

    ikiwemo kukamata viongozi wetu, kuanzisha mchakato wa katiba na kueneza

    uvumi na propaganda usio na ukweli wowote.

    6. JUMIKI itaendelea kusisitiza kama ni kuendelea na muungano au laa kwakuheshimiwa matakwa ya wananchi pia kupewa fursa ya kutoa maoni kwa

    mujibu wa Katiba ya Zanzibar. Jumuiya tayari imekusanya majina ya watu

    sitini elfu kwa niaba ya Wazanzibari kwa ajili ya kupeleka mbele agenda ya

    kudai kura ya maoni na kudai mustakbali wa nchi yetu ya Zanzibar.

    Wabill ah Taufiq

  • 7/28/2019 uamsho-press-conference-25-05-2013.pdf

    6/6

    6

    IMETOLEWA NA:

    OFISI YA KATIBU MKUU

    JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAM

    ZANZIBAR